OIC yaonya: Mpango wa Israel wa kuikalia kwa mabavu Gaza ni "jinai za kivita"
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i129336
Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imelaani vikali uamuzi wa Israel wa kukalia kwa mabavu Ukanda wa Gaza na kuwaondoa kwa nguvu karibu Wapalestina milioni moja kutoka Gaza City na maeneo ya kaskazini mwa kusini, na kuuita mpango huo kuwa ni "jinai dhidi ya ubinadamu."
(last modified 2025-08-09T16:04:42+00:00 )
Aug 09, 2025 10:30 UTC
  • OIC yaonya: Mpango wa Israel wa kuikalia kwa mabavu Gaza ni

Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imelaani vikali uamuzi wa Israel wa kukalia kwa mabavu Ukanda wa Gaza na kuwaondoa kwa nguvu karibu Wapalestina milioni moja kutoka Gaza City na maeneo ya kaskazini mwa kusini, na kuuita mpango huo kuwa ni "jinai dhidi ya ubinadamu."

OIC imezitaja hatua za Israel huko Gaza kama sehemu ya muundo mpana wa "mauaji ya halaiki, uharibifu, njaa na kuzingirwa."

Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imevitaja vitendo hivi kuwa ni "uvunjaji na ukiukaji wa wazi wa sheria ya kimataifa ya kibinadamu" na ukaidi wa maazimio ya Umoja wa Mataifa na maagizo ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki.

OIC imelitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuchukua hatua za haraka ili kupatikane usitishaji vita wa kudumu, kudhamini upatikanaji wa misaada ya kibinadamu bila vikwazo, na kutoa ulinzi wa kimataifa kwa Wapalestina.

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa, mpango wa Israel wa kuikalia kwa mabavu Gaza unapaswa kusitishwa mara moja.

Katika radiamali yake kwa uamuzi wa utawala haramu wa Israel wa kuikalia Gaza kwa mabavu, Volker Turk amesema, mpango huo unakinzana na uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki unaosema,  Israel lazima ikomeshe uvamizi wake haraka iwezekanavyo.

Liitwalo 'baraza la mawaziri la kisiasa na kiusalama' la utawala haramu wa kizayuni wa Israel limeidhinisha mpango wa waziri mkuu wa utawala huo ghasibu Benjamin Netanyahu wa kulikalia kwa mabavu eneo lote la Ukanda wa Ghaza kwa kuwahamisha kwanza kwa nguvu makumi ya maelfu ya Wapalestina wa Gaza City.