Ghaza yaandamwa na mashambulio ya kiwendawazimu ya Wazayuni, wanakaribia kuikalia kikamilifu
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i130860-ghaza_yaandamwa_na_mashambulio_ya_kiwendawazimu_ya_wazayuni_wanakaribia_kuikalia_kikamilifu
Jeshi la utawala wa kizayuni wa Israel limeanzisha mashambulizi makali ya anga dhidi ya Mji wa Ghaza kwa saa kadhaa, ambapo mbali na kuwaua shahidi Wapalestina kadhaa linateketeza pia majengo na miundomsingi iliyosalia katika eneo hilo.
(last modified 2025-10-15T09:12:33+00:00 )
Sep 16, 2025 07:03 UTC
  • Ghaza yaandamwa na mashambulio ya kiwendawazimu ya Wazayuni, wanakaribia kuikalia kikamilifu

Jeshi la utawala wa kizayuni wa Israel limeanzisha mashambulizi makali ya anga dhidi ya Mji wa Ghaza kwa saa kadhaa, ambapo mbali na kuwaua shahidi Wapalestina kadhaa linateketeza pia majengo na miundomsingi iliyosalia katika eneo hilo.

Gazeti la lugha ya Kiebrania la Yisrael Hayom limeripoti kuwa, nguvu ya mashambulizi hayo yanayofanywa dhidi ya Ghaza ni kali kiasi kwamba sauti ya miripuko inaweza kusikika mjini Tel Aviv.

Televisheni ya Al-Aqsa imeripoti kuwa wanajeshi wa utawala wa kizayuni wanashambulia kwa mabomu mji wa Ghaza kwa kutumia ndege, mizinga, helikopta na ndege zisizo na rubani. 

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, nguvu ya miripuko hiyo ni kubwa sana kiasi kwamba sauti zake zinaweza kusikika umbali wa zaidi ya kilomita 100.

Hayo yanajiri katika hali ambayo, duru za habari zimeripoti leo asubuhi kwamba jeshi la utawala ghasibu wa Israel linakaribia kuukalia kikamilifu Mji wa Ghaza kwa kisingizio cha kuiangamiza harakati ya Muqawama wa Kiislamu na ya ukombozi wa Palestina ya Hamas.

Kwa mujibu wa tovuti ya habari ya Axios, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio amemueleza Waziri Mkuu wa utawala wa kizayuni wa Israel Benjamin Netanyahu kwamba Washington inaunga mkono operesheni hiyo ya ardhini ya kuivamia na kuikalia kwa mabavu kikamilifu Ghaza, lakini inataka kuona inafanyika kwa kasi na kuhitimishwa haraka iwezekanavyo.

Hayo yanajiri katika hali ambayo, tangu mapambazuko ya leo hadi sasa, Wapalestina wasiopungua 24 wameuawa shahidi kutokana na mashambulio makali na ya kinyama yanayoendelea kufanywa na jeshi la Israel.../