Yemen yaingia rasmi vitani kwa maslahi ya Iran
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i137736-yemen_yaingia_rasmi_vitani_kwa_maslahi_ya_iran
Yemen imetangaza rasmi kuingia katika vita kwa maslahi ya Iran, na sasa kila mtu ana wasiwasi kuhusu muelekeo wa vita hivi huku Wamagharibi na waungaji mkono wa utawala ghasibu wa Israel wakiingiwa na wasi wasi mkubwa kwamba huenda uchumi wa utawala huo ukabanwa na kupata madhara makubwa iwapo jeshi la Yemen litaamua kufunga na kudhibiti njia muhimu ya usafiri wa meli za biashara na mizigo, yaani Lango-Bahari la Bab al-Mandab.
(last modified 2026-04-02T06:43:32+00:00 )
Apr 02, 2026 06:43 UTC
  • Yemen yaingia rasmi vitani kwa maslahi ya Iran

Yemen imetangaza rasmi kuingia katika vita kwa maslahi ya Iran, na sasa kila mtu ana wasiwasi kuhusu muelekeo wa vita hivi huku Wamagharibi na waungaji mkono wa utawala ghasibu wa Israel wakiingiwa na wasi wasi mkubwa kwamba huenda uchumi wa utawala huo ukabanwa na kupata madhara makubwa iwapo jeshi la Yemen litaamua kufunga na kudhibiti njia muhimu ya usafiri wa meli za biashara na mizigo, yaani Lango-Bahari la Bab al-Mandab.

Mbali na hayo lakini swali muhimu linaloulizwa kuhusiana na kadhia hii ni taathira za moja kwa moja za nafasi ya Yemen katika vita vinavyoendelea na kwamba je, kuingia Yemen vitani kutaathiri vipi milinganyo ya vita vya sasa?Ikiwa ni katika kujibu swali hili muhimu kwanza kabisa hatupasi kupuuza nguvu na uwezo wa makombora pamoja na ndege zisizokuwa na rubani za nchi hiyo kutika kubadilisha milingano ya nguvu na kijeshi katika medani ya vita.

Masafa ya kioperesheni ya makombora ya balestiki ya Yemen kama vile Palestina 2 au droni za Samaad-3 na Yafa za jeshi la Yemen yanafikia zaidi ya kilomita 2,000.Hii ina maana kuwa, mbali na ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu, vituo na meli za Marekani na Israel katika Bahari ya Hindi, Bahari Nyekundu, Afrika Kaskazini na hata Bahari ya Mediterania, hazitakuwa salama tena.Pili, ni Bab al-Mandab, sehemu ya kubanwa uchumi wa Israel. Takriban asilimia 80 ya nishati ya Israel inaagizwa kutoka nje, ambapo sehemu yake kubwa inapitia lango bahari hilo.

Kama tulivyoshuhudia katika miezi ya karibuni, na ikiwa ni katika kuunga mkono watu wa Ukanda wa Gaza wanaonyanyaswa na utawala wa kigaidi wa Israel, Harakati ya Ansarullah ya Yemen ambayo inadhibiti njia hiyo muhimu ya baharini iliweza kutoa pigo kubwa kwa meli za biashara za Wazayuni na nchi za Magharibi kwa ujumla, ambazo zinauunga mkono vitendo vya ugaidi na jinai za utawala huo na kutozirihusu kupitia lango bahari hilo jambo ambalo hatimaye lilipelekea nchi hizo na hasa Marekani kusalimu amri mbele ya matakwa ya Ansarullah na jeshi la Yemen.Mwaka 2023 pekee, takriban tani milioni 100 za bidhaa ziliingizwa Israel kupitia njia hiyo.

Askari wa Yemen wakitua na kudhibiti moja ya meli za adui katika lango la Babul Mandab

 

Sasa, kwa kuingia Yemen vitani, njia hii pia haitakuwa salama kwa utawala huo.Suala la tatu muhimu kuhusu nguvu na nafasi ya Yemen kuingia katika vita vya hivi sasa  ni uzoefu wake wa miaka iliyopita katika medani ya vita hasa hasa linapokuja suala la  vita na  mapigano ya nchi kavu. Yemen ni nchi ambayo imekuwa katika vita vya moja kwa moja na muungano wa Saudia na Imarati kwa msaada wa Marekani, kwa miaka mingi. Kinyume na zilivyo nchi nyingi za Kiarabu ambazo ni vibaraka wa nchi za Magharibi na hasa Marekani, ambazo zimeruhusiwa kuweka vituo vyao vya kijeshi katika ardhi za nchi hizo kwa madhumuni ya kuhujumu nchi za kiislamu, Yemen ambayo inaoongozwa na Ansarullah imekataa kufuata mkono huo na kuamua kulinda heshima na uhuru wa kujiamulia mambo yake yenyewe.

Imethibitisha kivitendo kuwa ina uwezo sio tu katika kujitetea, bali pia katika kushambulia adui na kumsababishia hasara kubwa. Swali jingine muhimu linaloulizwa na wengi ni kwamba, je, Marekani na Israel zina uwezo wa kusimamisha mapambano ya mrengo wa Yemen?Swali hili linajibiwa kirahisi tunaporejea nyuma kidogo na kutathmini matukio ya baada ya Oktoba 7, 2023 na kuanza operesheni za Ansarullah za kuwatetea watu wa Gaza, ambapo Marekani ililazimika kuunda muungano wa kijeshi wa wanamaji wa zaidi ya nchi 20 ili kuidhibiti Yemen na mashambulio makali ya kundi hilo muhimu la mapambano la mrengo wa muqawama.Kila mtu anajua vizuri matokeo ya hatua hiyo ya Marekani.

Licha ya juhudi zote zilizofanywa na Washington katika uwanja huo lakini si tu kwamba mashambulizi ya Yemen dhidi ya Israel na udhibiti wa Bab al-Mandab havikusimama, bali pia kushindwa kwa vikosi vya jeshi la anga na majini vya Marekani na NATO kulionekana wazi mbele ya kila mtu. Hivyo, kuingia Yemen vitani sio onyesho tu la kijeshi na usalama bali ni hatua muhimu inayoweza kutoa mchango mkubwa katika kutoa mashinikizo dhidi ya pande chokozi zilizoanzisha hujuma ya kijeshi dhidi ya Iran na hivyo kuharakisha mkondo wa kushindwa Marekani na Israel katika eneo zima la Asia Magharibi.