Majeshi ya Yemen yakabiliana na mamluki wa Saudia mkoani Ta’izz
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i141208-majeshi_ya_yemen_yakabiliana_na_mamluki_wa_saudia_mkoani_ta’izz
Inaripotiwa kuwa maelfu ya mamluki wanaofadhiliwa na ufalme wa Saudi Arabia wamekabiliana na Majeshi ya Yemen katika mkoa wa Ta’izz.
(last modified 2026-09-05T03:02:23+00:00 )
Sep 05, 2026 02:59 UTC
  • Majeshi ya Yemen yakabiliana na mamluki wa Saudia mkoani Ta’izz
    Majeshi ya Yemen yakabiliana na mamluki wa Saudia mkoani Ta’izz

Inaripotiwa kuwa maelfu ya mamluki wanaofadhiliwa na ufalme wa Saudi Arabia wamekabiliana na Majeshi ya Yemen katika mkoa wa Ta’izz.

Taarifa zinasema Majeshi ya Yemen yamepata mafanikio makubwa ya kijeshi katika kukabiliana na mamluki hao huku yakichukua udhibiti wa maeneo mapana ya mkoa huo na kusonga kuelekea bandari ya al-Mokha.

Imedokezwa kuwa angalau mamluki 39 wanaofadhiliwa na Saudia, wakiwemo makamanda waandamizi, wameuawa katika mapigano mapya yaliyoanza Alhamisi.

Majeshi ya Yemen, yakitumia makombora na droni, yametekeleza shambulio la nchi kavu karibu na pwani ya Al Mokha katika Bahari ya Sham na maeneo ya jirani ya Ta’izz siku ya Alhamisi.

Vyanzo pia vilitangaza mashambulizi mapya ya Majeshi ya Yemen dhidi ya bandari ya al-Mokha, ambayo ni moja ya njia kuu za kuingiza silaha na vifaa kwa ajili ya mamluki hao.

Katika miezi ya hivi karibuni, bandari hiyo imekuwa lengo la makumi ya mashambulizi ya makombora na droni ya Majeshi Yemen. Bandai ya al Mokha ipo kwenye Bahari ya Sham karibu na Bab al-Mandab, njia muhimu ya kimkakati kwa sehemu kubwa ya biashara ya bahari duniani.

Mapigano katika pwani ya Magharibi ya Yemen ni miongoni mwa makali zaidi katika miaka ya hivi karibuni.

Mapigano haya pia yanakuja wakati majeshi ya Yemen yakiongeza mashambulizi yao ya kulipiza kisasi dhidi ya malengo muhimu nchini Saudi Arabia.

Kwa takriban muongo mmoja, Saudia imetekeleza mzingiro mkubwa wa nchi kavu, bahari, na anga dhidi ya Yemen. Umoja wa Mataifa umeuelezea mzingiro huowa kuwa chanzo kikuu cha mgogoro mbaya zaidi wa kibinadamu duniani. Mzingiro huo unalenga kwa makusudi uwezo wa Yemen kuingiza chakula, mafuta, na dawa, huku wakati huo huo ukijaribu kuiba rasilimali za mafuta na gesi za taifa hilo.

Kwa kutumia uwezo wake mkubwa wa kijeshi ikiwemo droni na makombora, Yemen imehama kutoka katika nafasi ya ulinzi tu na kuwa katika kampeni ya hujuma. Mkakati huu umeundwa ili kuleta gharama za moja kwa moja za kiuchumi na kijeshi kwa utawala wa Saudi ili uondoe mzingiro, usitishe vite na urejeshe a mamlaka kamili ya Yemen kujitawala.