Kuzidi kutengwa Israel katika uga wa kimataifa
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i15229-kuzidi_kutengwa_israel_katika_uga_wa_kimataifa
Habari mbalimbali kutoka barani Ulaya zinaeleza kuwa kumekuwepo muelekeo mkubwa zaidi katika bara hilo wa kuususia na kuuwekea vikwazo zaidi utawala wa Kizayuni wa Israel.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 13, 2016 03:07 UTC
  • Kuzidi kutengwa Israel katika uga wa kimataifa

Habari mbalimbali kutoka barani Ulaya zinaeleza kuwa kumekuwepo muelekeo mkubwa zaidi katika bara hilo wa kuususia na kuuwekea vikwazo zaidi utawala wa Kizayuni wa Israel.

Kuhusiana na suala hilo, sambamba na kutangazwa habari ya kujiunga miji na majimbo zaidi ya 50 ya Uhispania na harakati ya kimataifa ya kuisusia Israel, imeripotiwa kwamba idadi kadhaa ya wabunge wa Bunge la Ulaya wametaka klabu za soka za utawala huo haramu zifungiwe kushiriki mashindano ya soka ya barani Ulaya.

Harakati ya kuisusia Israel kiuchumi

Harakati ya kimataifa ya kuisusia Israel inayoungwa mkono na jumuiya mbalimbali za biashara, makundi ya kidini, mashirika yasiyo ya kiserikali, serikali za wananchi na asasi za kiraia ulimwenguni kote inazidi kupanuka; na ususiaji na vikwazo ulivyowekewa utawala wa Kizayuni vimekuwa na taathira kubwa kisiasa, kidiplomasia, kiutamaduni, kiuchumi na hata kimichezo kwa utawala huo ghasibu.Katika kuendeleza kampeni hiyo, wabunge 66 wa Bunge la Ulaya wamemwandikia barua Gianni Infantino, Rais wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) wakitaka klabu za soka za Israel na za vitongoji vya walowezi wa Kizayuni ambao kulingana na sheria za kimataifa na maazimio ya Umoja wa Mataifa kuishi na kuwepo kwao katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu ni kinyume cha sheria, zifungiwe kushiriki mashindano ya kimataifa ya soka.

Rais wa FIFA Gianni Infantino

Kitambo nyuma makundi mbalimbali ya Kipalestina yalimwandikia barua Rais wa FIFA yakimtaka aifungie timu ya taifa ya utawala wa Kizayuni kushiriki mashindano ya kimataifa ya mchezo huo.

Ombi la Wapalestina la kutaka kususiwa zaidi utawala wa Kizayuni na kupigania kusimamishwa uanachama wa Israel katika Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limewatia kiwewe viongozi wa utawala huo haramu, kiasi kwamba Rais wa Israel Reuven Rivlin amenukuliwa akisema, hatua za aina hiyo ni tishio la kistratijia na hatari kwa utawala huo wa Kizayuni.

Reuven Rivlin, Rais wa utawala wa Kizayuni wa Israel

Hakuna shaka yoyote kuwa hatua iliyochukuliwa katika miaka ya karibuni katika mashindano ya kimataifa na wanamichezo wengi kutoka nchi za Kiislamu na za Kiarabu ya kukataa kupambana na wanamichezo wenye uraia wa utawala unaoikalia Quds kwa mabavu imedhihirisha kwa uwazi zaidi ukubwa wa hasira na chuki zilizoongezeka kimataifa dhidi ya utawala haramu wa Kizayuni.

Hayati Nelson Mandela, alikuwa mmoja wa watetezi wa haki za Wapalestina kimataifa

Nukta ya kutaamali na kuzingatia ni kwamba, katika mgawanyo wa kijiografia katika uga wa michezo, Israel imewekwa kwenye bara la Ulaya, suala linaloonyesha wazi kuwa utawala huo ni bandia na hauna uhalali wowote kisheria mbele ya mataifa ya eneo la Mashariki ya Kati na bara la Asia kwa ujumla. Japokuwa Israel nzima iko kwenye eneo la Mashariki ya Kati lililoko katika bara la Asia lakini kutokana na uanachama wa utawala huo bandia kususiwa kwa miongo kadhaa na Waarabu na hasa Waislamu katika Shirikisho la Soka la Asia, mnamo mwaka 1994 Israel ilijiunga na Shirikisho la Soka la Ulaya (UEFA). 

Hata hivyo kujiunga utawala haramu wa Israel na UEFA nako pia hakujaweza kupunguza moto wa chuki za Jamii ya Kimataifa unaouwakia utawala huo haramu; na miito mingi ambayo imekuwa ikitolewa huko Ulaya kutaka utawala huo upigwe marufuku kushiriki mashindano ya michezo ya barani humo na ya kimataifa ni ithbati na ushahidi tosha wa kushamiri wimbi la upinzani na malalamiko dhidi ya Israel na kuzidi kusambaa wimbi hilo hadi barani Ulaya.

Kampeni za kususia bidhaa za utawala haramu wa Israel

Misimamo na radiamali zinazoonyeshwa kimataifa dhidi ya utawala wa Kizayuni na sisitizo la kimataifa la kutaka kutekelezwa vikwazo dhidi ya utawala huo ni sawa na kusema kwamba uga wa kimataifa sasa unabadilika kuwa vuguvugu na harakati kubwa dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel.../