Saudia kununua silaha zaidi kutoka Ukraine
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i18460-saudia_kununua_silaha_zaidi_kutoka_ukraine
Utawala wa kifalme wa Saudi Arabia umeongeza ushirikiano wake na nchi ya Ulaya Mashariki ya Ukraine na iko mbioni kununua silaha zaidi kutoka nchini humo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 30, 2016 11:55 UTC
  • Saudia kununua silaha zaidi kutoka Ukraine

Utawala wa kifalme wa Saudi Arabia umeongeza ushirikiano wake na nchi ya Ulaya Mashariki ya Ukraine na iko mbioni kununua silaha zaidi kutoka nchini humo.

Gazeti la al Akhabar la nchini Lebanon limechapisha nyaraka kadhaa leo Jumapili na kusema kwamba, inavyoonekana ni kuwa utawala wa Aal Saud una ajenda ya kupanua ushirikiano wake wa kijeshi na nchi mbalimbali na hivi sasa uko mbioni kununua silaha kutoka nchini Ukraine.

Kwa mujibu wa nyaraka hizo, ushirikiano baina ya Kiev na Riyadh umejikita katika teknolojia ya makombora na mifumo ya anga.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, viwanda vya kijeshi, makombora na masuala ya anga vya Ukraine, hivi karibuni viliipa Saudia pendekezo la kununua makombora ya masafa ya mbali ya Balestiki kutoka nchini humo.

Saudia inatumia silaha inazopewa na madola ya kibeberu kufanya mauaji dhidi ya Waislamu wa Yemen

 

Kwa mujibu wa gazeti hilo, hivi sasa Saudi Arabia ndiye mnunuzi mkubwa wa silaha duniani. Mwaka jana 2015, nchi hiyo ilinunua silaha zenye thamani ya zaidi ya dola bilioni 9 ikiwa ni ongezeko la zaidi ya asilimia 50 ikilinganishwa na mwaka wa kabla yake, yaani 2014.

Mashambulizi dhidi ya wananchi wa Yemen na kuyasaidia kwa silaha magenge ya kigaidi yanayofanya mauaji katika baadhi ya nchi za Mashariki ya Kati ndiko kulikoifanya Saudia kuwa mnunuzi mkubwa wa silaha ulimwenguni.