WHO: Maelfu ya watu wameuawa nchini Yemen
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i18985-who_maelfu_ya_watu_wameuawa_nchini_yemen
Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa maelfu ya watu wameuawa nchini Yemen katika mashambulizi ya Saudi Arabia na washirika wake ambayo yanaingia mwezi wa 20 sasa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 07, 2016 11:20 UTC
  • WHO: Maelfu ya watu wameuawa nchini Yemen

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa maelfu ya watu wameuawa nchini Yemen katika mashambulizi ya Saudi Arabia na washirika wake ambayo yanaingia mwezi wa 20 sasa.

Taarifa ya WHO imesema kuwa, zaidi ya raia elfu 7 wameuawa katika mashambulizi ya Saudia nchini Yemen na kwamba watu wengine milioni 21 wa nchi hiyo wanahitajia misaada ya dharura ya kitiba.

Taarifa ya shirika hilo la Umoja wa Mataifa imeongeza kuwa, Wayemeni milioni mbili na laki moja wamepoteza nyumba na mazi yao katika mashambulizi ya Saudia na kwamba zaidi ya nusu ya hospitali na vituo vya tiba kote nchini Yemen vimesimamisha kazi kwa kuharibiwa au vimepunguza kabisa shughuli zao.

Mtoto wa Yemen akiwa kwenye mabaki ya nyumba iliyoshambuliwa na Saudia

Majeshi ya Saudi Arabia na washirika wake kama Marekani, Israel na nchi kadhaa za Kiarabu, yalianza kushambulia taifa la Yemen mwezi Machi mwaka jana kwa kisingizio cha kumrejesha madarakani rais aliyetoroka nchi na kukimbilia Saudia, Abd Rabbuh Mansur Hadi.