Wapalestina wengi wanataka Mahmoud Abbas ajiuzulu
Uchunguzi wa maoni uliofanywa unaonyesha kuwa asilimia 64 ya Wapalestina wanataka Mahmoud Abbas, Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina ajiuzulu.
Kwa mujibu wa uchunguzi huo wa maoni uliofanywa katika Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan kati ya tarehe 11 hadi 18 ya mwezi huu wa Machi, ni asilimia 31 tu ya waliotoa maoni yao wanataka Mahmoud Abbas aendelee kuwa Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina.
Aidha kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa hivi karibuni, akthari ya Wapalestina wanakosoa misimamo ya kiadui ya viongozi wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina dhidi ya muqawama inayochukuliwa kwa sababu ya upinzani mkali wa muqawama huo dhidi ya wimbi jipya la ujenzi wa vitongoji haramu unaofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel.
Wapalestina wanasisitiza kuwa jibu mwafaka kwa mipango ya ujenzi wa vitongoji ni kusimamishwa ushirikiano wa kiusalama baina ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina na Israel na viongozi wa Palestina kuwasilisha mashtaka katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai kuhusiana na suala hilo.
Wananchi na makundi ya wanamapambano wa Palestina wanaitakidi kuwa ushirikiano na uratibu wa kiusalama uliopo kati ya Mamlaka ya Ndani na Israel ni hatari kubwa kwa Wapalestina; na kuendeleza mazungumzo ya mapatano na Wazayuni kila mara kumekuwa na madhara kwa wananchi hao madhulumu.../