Vikosi vya Israel vyawateka nyara Wapalestina 14 Ukingo wa Magharibi
Vikosi katili vya utawala wa Kizayuni wa Israel vimewateka nyara raia 14 wa Palestina katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
Katika uvamizi uliofanywa jana Jumapili na askari katili wa Israel, Wapalestina 14 walimakatwa katika miji ya al-Khalil, Baitu Lahm, Quds tukufu na Jenin.
Habari zaidi zinasema kuwa, raia wa Kipalestina waliotekwa nyara katika operesheni hiyo ya jana ya jeshi la utawala haramu wa Israel ni pamoja na wanawake na watoto.

Kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa, vikosi katili vya utawala khabithi wa Israel vilifanya operesheni za kivamizi karibu 95 kwa wiki mwaka uliopita 2016.
Mapema mwezi huu, ripoti ya kituo cha Palestinian Prisoners’ Center for Studies ilifichua kuwa, takriban Wapalestina 420 wametiwa mbaroni na askari wa utawala wa Kizayuni wa Israel mwezi uliopita wa Februari pekee.
Zaidi ya Wapalestina elfu 7 wanazuilia chini ya mazingira magumu, mateso na udhalilishaji katika jela na korokoro za utawala pandikizi wa Israel.