UN yapasisha maazimio kuilaani Israel, kuiunga mkono Palestina
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i26828-un_yapasisha_maazimio_kuilaani_israel_kuiunga_mkono_palestina
Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa limepasisha maazimio manne ya kuliunga mkono taifa la Palestina na kuulaani utawala ghasibu wa Israel.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 25, 2017 01:58 UTC
  • UN yapasisha maazimio kuilaani Israel, kuiunga mkono Palestina

Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa limepasisha maazimio manne ya kuliunga mkono taifa la Palestina na kuulaani utawala ghasibu wa Israel.

Katika maazimio hayo yaliyopitishwa kwa wingi wa kura katika kikao cha 34 cha baraza hilo mjini Geneva,  utawala wa Kizayuni wa Israel ulilaaniwa kwa kukiuka haki za Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Ukanda wa Ghaza. Aidha Israel ililaaniwa kwa kujenga vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika Ukingo wa Magharibi. Halikadhalika baraza hilo lilikosoa hali ya haki za binadamu katika aradhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Israel sambamba na kuunga mkono haki ya Wapalestina ya kuainisha hatima ya taifa lao.

Wapalestina wanaweza kutumia maazimio hayo kuushtaki utawala wa Kizayuni wa Israel katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC. 

Shahidi Mazen Fuqaha

Katika upande mwingine, Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel zilijaribu pasina kufanikiwa kuzishawishi nchi wanachama kuzuia kupasishwa azimio hilo.

Huku hayo yakijiri utawala wa Kizayuni wa Israel umeendeleza ugaidi wake wa kiserikali kwa kumuua afisa mwandamizi wa harakati ya Hamas huko Ghaza. Duru zinasema watu waliokuwa na silaha jana usiku walimpiga risasi na kumuua shahidi Mazen Fuuqaha mmoja wa viongozi wa ngazi za juu wa Hamas katika Ukanda wa Ghaza.