Iran, Uturuki na Qatar zajadili namna ya kuimarisha uhusiano wa kibiashara
(last modified Sun, 06 Aug 2017 07:22:59 GMT )
Aug 06, 2017 07:22 UTC
  • Iran, Uturuki na Qatar zajadili namna ya kuimarisha uhusiano wa kibiashara

Mawaziri watatu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Qatar na Uturuki wamefanya mkutano hapa mjini Tehran na kuzungumzia mikakati ya kuimarisha uhusiano wa kibiashara wa pande tatu.

Mkutano huo wa pande tatu umehudhuriwa na Mahmoud Vaezi, Waziri wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ya Iran, Nihat Zeybekci, Waziri wa Uchumi wa Uturuki na mwenzake wa Qatar, Ahmed bin Jassim Al Thani.

Mbali na kujadili kadhi ya kuimarisha uhusiano na ushirikiano wa kibiashara miongoni mwa Tehran, Doha na Ankara, mawaziri hao wamesisitiza pia umuhimu wa kuwekwa mikakati ya kufanikisha kutumwa biadhaa za Uturuki nchini Qatar kupitia Iran.

Bendera za nchi za Kiarabu zilizoiwekea Qatar vikwazo

Saudi Arabia, Imarati, Bahrain na Misri tarehe 5 mwezi Juni mwaka huu ziliiwekea vikwazo vya nchi kavu, angani na habarini Qatar baada ya kutangaza kukata uhusiano wao wa kidiplomasia na nchi hiyo. 

Iran na Uturuki zimekuwa wasafirishaji wakubwa wa bidhaa zinazohitajika Qatar baada ya Doha kuwekewa vikwazo kwa tuhuma kuwa inaunga mkono na kafadhili magenge ya kigaidi.

Tags