Kukosolewa siasa za Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Yemen
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i3655-kukosolewa_siasa_za_mjumbe_wa_umoja_wa_mataifa_nchini_yemen
Harakati ya Ansarullah ya Yemen imekosoa siasa zinazotekelezwa na Mjumbe wa Umoja wa Mataifa kuhusiana na mgogoro wa nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 23, 2016 10:32 UTC
  • Kukosolewa siasa za Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Yemen

Harakati ya Ansarullah ya Yemen imekosoa siasa zinazotekelezwa na Mjumbe wa Umoja wa Mataifa kuhusiana na mgogoro wa nchi hiyo.

Muhammad al Bakhiti Mwakilishi wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Wananchi ya Ansarullah ya Yemen amemtuhumu Ismail Ould Sheikh Ahmad Mjumbe wa Umoja wa Mataifa katika Masuala ya Yemen kwa kuikingia kifua Saudi Arabia. Muhammad al Bakhiti amesema kuwa Ismail Ould Sheikh Ahmad anaegemea upande mmoja na kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa siasa za Saudi Arabia.

Mwkailishi wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Harakati ya Ansarullah ya Yemen amekanusha baadhi ya taarifa kwamba mazungumzo ya amani ya Yemen yatafanyika tarehe 17 mwezi Aprili na kusisitiza kuwa tarehe ya kufanyika mazungumzo hayo bado haijaainishwa.

Shirika la habari la Reuters jana lilimnukuu afisa mmoja wa serikali iliyojiuzulu ya Yemen na kudai kuwa mazungumzo ya amani ya nchi hiyo yatafanyika Kuwait tarehe 17 mwezi Aprili.