Mar 26, 2016 01:42 UTC
  • Wabahrain watano wavuliwa uraia na kuhukumiwa kifungo jela

Mahakama moja nchini Bahrain imewahukumu vifungo vya miaka mitano hadi 15 jela wapinzani wa utawala wa ukoo wa Aal Khalifa.

Mahakama ya Jinai ya Bahrain imewavua uraia wananchi hao kwa tuhuma za kujiunga na Muungano wa Februari 14 wa vijana wanaoupinga utawala wa kidikteta wa Aal Khalifa.

Ripoti kutoka Manama zinaeleza kuwa mahakama ya jinai ya Bahrain imewahukumu pia washtakiwa wawili kati ya watatu kifungo cha miaka 15 jela na faini ya dinari laki moja na kutoa hukumu ya kifungo cha miaka mitano jela kwa washtakiwa wengine wawili.

Wataalamu wengi wa sheria wanaamini kuwa vyombo vya mahakama nchini Bahrain havina uhuru unaohitajika bali vina mfungamano na utegemezi kwa utawala wa Aal Khalifa.

Siku ya Alkhamisi pia mahakama ya Bahrain iliwahukumu vifungo vya kati ya miaka saba hadi 10 jela watu saba kwa tuhuma za kuvuruga amani kando ya jengo la Wizara ya Mambo ya Ndani.

Kituo cha haki za binadamu cha Bahrain kimetoa taarifa na kueleza kwamba tangu tarehe 14 hadi 20 mwezi huu wa Machi askari wa utawala wa Aal Khalifa wamewatia nguvuni watu 22 miongoni mwao wakiwemo wanawake na watoto.../

Tags