Mwaka 2017; Israel iliwauwa shahidi watoto 15 wa Kipalestina
(last modified Wed, 10 Jan 2018 07:43:54 GMT )
Jan 10, 2018 07:43 UTC
  • Mwaka 2017; Israel iliwauwa shahidi watoto 15 wa Kipalestina

Harakati ya Kimataifa ya Kuwatetea Watoto tawi la Palestina imetangaza kuwa wanajeshi wa utawala wa Kizayuni mwaka uliopita wa 2017 uliwauwa shahidi watoto 15 wa Kipalestina katika eneo la Ukanda wa Ghaza, Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Quds.

Harakati hiyo imesema katika taarifa yake iliyoitoa wiki hii kwamba mwaka jana wa 2017 watoto 12 wa Kipalestina walikufa shahidi kwa kupigwa risasi na Wazayuni; ambapo wanne waliuawa katika mapigano kati yao na wanajeshi wa Kizayuni, watoto watatu waliuliwa baada ya kuviziwa na wanajeshi wa utawala huo na watano wengine waliuawa shahidi baada ya Wazayuni kudai kuwa watoto hao walikuwa wakijaribu kutekeleza oparesheni za kimuqawama. 

Watoto watatu wengine wa Kipalestina waliuawa shahidi katika mashambulizi ya jeshi la utawala wa Kizayuni katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Ukanda wa Ghaza. 

Katika upande mwingine, Riyadh al Ashqar msemaji wa kituo cha utafiti cha mateka wa Palestina ametangaza kuwa maghasibu wa Kizayuni mwaka jana waliwatia mbaroni wanawake na watoto wa Kipalestina wasiopungua 170. Amesisitiza kuwa jeshi la Israel mwaka jana lilishadidisha kuwatia nguvuni na kuwakandamiza wanawake na mabinti wa Kipalestina ili kuwazuia kushiriki katika mapambano na muqawama dhidi ya Wazayuni.  

Ukandamizaji na utiaji mbaroni wa wanawake wa Kipalestina unaofanywa na wanajeshi wa Israel

 

Tags