Tsunami ya ufisadi ndani ya utawala haramu wa Israel
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i41181-tsunami_ya_ufisadi_ndani_ya_utawala_haramu_wa_israel
Tangu ulipoanzishwa utawala haramu wa Israel viongozi kadhaa wa utawala huo wamewekwa jela kutokana na ufisadi wa aina mbalimbali ukiwemo ufisadi wa kifedha.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 05, 2018 00:31 UTC
  • Tsunami ya ufisadi ndani ya utawala haramu wa Israel

Tangu ulipoanzishwa utawala haramu wa Israel viongozi kadhaa wa utawala huo wamewekwa jela kutokana na ufisadi wa aina mbalimbali ukiwemo ufisadi wa kifedha.

Benjamin Netanyahu, Ehud Barak, Ariel Sharon na Ehud Olmert, ni miongoni mwa mawaziri wakuu wa Israel ambao wamewahi kusailiwa na polisi ya utawala huo bandia kutokana na ufisadi wa kifedha. Moshe Katsav, rais wa zamani wa Israel naye pia alifungwa jela kutokana na ufisadi wa kimaadili. Mbali na hapo ni kwamba, David Ben-Gurion, alikuwa waziri mkuu wa kwanza wa utawala haramu wa Israel kukabiliwa na tuhuma za ufisadi baada ya kummkingia kifua mtoto wake wa kiume, Amos kutokana na ufisadi wake wa kifedha. Aidha mawaziri wakuu wa baada ya Ben-Gurion akiwemo Yitzhak Rabin na Menachem Begin nao walikumbwa na zimwi hilo hilo la ufisadi na ubadhirifu wa mali ya umma huko Israel.

Ariel Sharon, waziri mkuu wa zamani wa Israel ambaye naye alikuwa kinara wa ufisadi

Kufuatia hali hiyo siku chache zilizopita gazeti la utawala huo la Haaretz liliandika kwamba: “Mbali na mawaziri wakuu wa sasa wa Israel, akthari ya viongozi wa ngazi mbalimbali wakiwemo wawakilishi wa Bunge la Israel (Knesset) na kadhalika mawaziri, wamesailiwa na vyombo husika kutokana na ufisadi wa kiuchumi na ufuska unaowakabili.” Gazeti hilo lilikiri kwamba, ufisadi ni jambo lililokita mizizi ndani ya muundo wa kisiasa wa Israel.

Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa sasa wa Israel anakabiliwa na mafaili kadhaa ya ufisadi wa kifedha na kupokea rushwa na karibu kila wiki Waisraeli wamekuwa wakifanya maandamano kwa lengo la kumshinikiza waziri mkuu huyo ang’atuke madarakani.

Benjamin Netanyahu na Ehud Barak kushoto ambao wote wanaandamwa na tuhuma lukuki za ufisadi

Hayo yanajiri katika hali ambayo, Netanyahu na mke wake, Miriam Weizmann tayari wameshasailiwa na polisi ya Israel kwa faili la ufisadi linalopewa jina la ‘Faili la 4000’.

Utawala wa Kizayuni ambao ni utawala vamizi na unaotambuliwa kimataifa kuwa dhidi ya ubinadamu unakabiliwa na aina mbalimbali za ufisadi na kimsingi tunaweza kusema kuwa, ufisadi ni moja ya sifa muhimu za utambulisho wa utawala huo khabithi. Mbali na hayo ni kwamba, ufisadi ni kadhia ambayo imekita mizizi hata ndani ya jamii ya utawala huo wa Israel na jambo ambalo limeenea kila kona. Si hayo tu, bali ufisadi katika jamii ya Kizayuni hususan miongoni mwa viongozi wake sio jambo la kuchukiza, na kinyume chake unatambuliwa kuwa ni jambo la kujifakharisha nalo.

Ehud Olmert, waziri mkuu wa Israel ambaye naye bado ana rundo la tuhuma za ufisadi

Kukithiri ufuska na ufisadi ndani ya jamii ya Israel, kunabainisha upana wa suala hilo katika ngazi ya utawala huo bandia ambao uliundwa na magenge na taasisi zilizozama katika ufisadi, uovu na kila aina ya ufuska. Karibu viongozi wote wa utawala wa Kizayuni na kutoka kila chama na makundi, wanakabiliwa na tuhuma za mafaili tofauti ya ufisadi na ufuska. Suala hilo pamoja na mambo mengine linabainisha kwamba waasisi na viongozi wa utawala huo katili wametokana na kundi la watu waovu na matokeo ya hali hiyo ni kuzaliwa jamii ya Kizayuni iliyoambukizwa aina mbalimbali ya maradhi ya ufisadi na uhalifu, mambo ambayo yanadhihirisha sura ya kuchukiza ya utawala huo. Kwa hakika ufisadi ni maafa makubwa ambayo yanatosha kusambaratisha jamii yoyote hususan jamii bandia kama ya Israel. Ufisadi  huo umezidisha hitilafu za kimatabaka, vinyongo na chuki kati ya raia wa utawala huo na hivyo kuchochea hujuma na misuguano ya mara kwa mara kati ya watu wake.

Israel, utawala unaoelekea kusambaratika

Wakati hali ya uaminifu kati ya watu wa jamii fulani na serikali inaposambaratika na mahusiano ya pande mbili yakajengeka juu ya msingi wa shaka na kutoaminiana, shughuli mbalimbali za kijamii na ushirikiano wa pande zote pia unasambaratika na hivyo kungamiza serikali au utawala husika. Hali hiyo ndiyo inayoshuhudiwa katika jamii ya kifisadi ya Israel na ni kwa kuzingatia suala hilo ndio maana hata weledi wa mambo na viongozi mbalimbali wa utawala huo khabithi akiwemo Avraham Burg, spika wa zamani wa Bunge la Israel wakakiri kuhusu kuwepo viashiria vya kusambaratika kikamilifu utawala huo. Alaa kullihal, aina mbalimbali za ufisadi, uovu na ufuska zinazidi kubainisha ubaya na sura halisi ya utawala huo wa Israel.