Kuingia wanajeshi wa Uturuki mjini Afrin, Syria na changamoto zitakazoibuka
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i41875-kuingia_wanajeshi_wa_uturuki_mjini_afrin_syria_na_changamoto_zitakazoibuka
Rais Reccep Tayyip Erdogan wa Uturuki jana alitangaza kuwa wanajeshi wa nchi yake sasa wamechukua udhibiti wa mji wa Afrin kaskazini mwa Syria.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 19, 2018 04:01 UTC
  • Kuingia wanajeshi wa Uturuki mjini Afrin, Syria na changamoto zitakazoibuka

Rais Reccep Tayyip Erdogan wa Uturuki jana alitangaza kuwa wanajeshi wa nchi yake sasa wamechukua udhibiti wa mji wa Afrin kaskazini mwa Syria.

Erdogan aliongeza kuwa: "Katika siku ya 28 tokea kuanza oparehseni inayojulikana kama Tawi la Mzaituni, makao makuu ya mji wa Afrin yalikuwa yamedhibitiwa kikamilifu na askari wa Uturuki.''

Erdogan amesema wanajeshi wa Uturuki wakishirikiana na wanamgambo wanaojiita 'Jeshi Huru la Syria' wameudhubiti kikamilifu mji wa Afrin.

Duru za habari zinasema Jeshi la Uturuki, asubuhu Jumapili lilichukua udhibiti  wa eneo kubwa la mji wa Afrin hadi katika eneo la kati kati mwa mji huo. Wakuu wa mji huo wanasema katika kipindi cha siku chache zilizopita, wakazi wasiopungua 150,000 wa mji huo walilazimika kukimbia makazi yao kufuatia hujuma ya jeshi la Uturuki.

Jeshi la Uturuki, kwa kisingizio cha kukabiliana na wanamgambo wapinzani wa Kikurdi, mnamo tarehe 20 Januari mwaka huu lilianzisha hujuma ya wazi dhidi ya Syria na likiwa linashirikiana na wanamgambo wanaojiita, 'Jeshi Huru la Syria', kwa lengo la kuchukua udhibiti wa  mji huo wa kaskazini mwa Syria.

Wanajeshi wa Uturuki wakiwa Afrin, Syria

Hivi sasa serikali ya Uturuki imefanikiwa kuingia katika mji wa Afrin na sasa maswali yanayoulizwa ni haya kuwa, je, hatua inayofuata ya Jeshi la Uturuki ni ipi? Na je, Jeshi la Uturuki litasitisha oparesheni yake au linatafakari kueneza wigo wa oparesheni zake nchini Syria?

Mwanzoni mwa 'Oparesheni za Tawi la Mzaituni' Uturuki ilikuwa ikisisitiza kuwa oparesheni hiyo ina muda maalumu na itaishia katika eneo maalumu la kijiografia. Inaelekea kuwa sera hiyo ilikuwa imetangazwa tu kwa ajili ya kupunguza upinzani na ukosoaji wa kimataifa. Hii ni kwa sababu hivi sasa wakuu wa Uturuki wanaashiria kuhusu kueneza oparsheni yao ya kijeshi katika maeneo mengine ya kaskazini mwa Syria. Kumeshuhudiwa ongezeko la askari wa Uturuki wenye silaha nzito nzito walio kaskazini mwa Syria na jambo hilo linaashiria kuenea zaidi oparesheni ya kijeshi baada ya kutekwa mji wa Afrin.

Aaron Stein, mtaalamu wa masuala ya Uturuki anasema: "Hivi karibuni Uturuki itachukua udhibiti wa maeeneo makubwa inayotaka kaskazini mwa Syria, na hakuna ushahidi wa kuoneysha kuwa askari wa Uturuki wataondoka katika ardhi ya Syria katika mustakabali wa karibu."

Wanamgambo wa PKK wa Kikurdi ambao Uturuki inasema inataka kuzuia ushawishi wao Syria

Hatua kama hivo bila shaka itakuwa ni ukiukwaji wa mamlaka ya kujitawala Syria mbali na kuwa ni upuuzaji wa wazi wa sheria za kimataifa. Aidha hali hiyo itapelekea kuongezeka idadi ya askari wa Uturuki wanaouawa na pia kuna raia wengi wasio na hatia watakaopoteza maisha katika eneo hilo.

Kuna udharura kwa Uturuki kungatia nukta hii kuwa, nchi za eneo zitaanza kuitazama kama mvamizi na mkaliaji mabavu wa ardhi ya Syria. Hali kama hii inaweza kupelekea kuibuka mgogoro na matatizo mengi ndani ya Uturuki yenyewe.

Kwa hivyo kuheshimu mamlaka ya kijitawala ardhi ya Syria na kuzingatia maslahi ya eneo sambamba na kutilia mkazo suala za haki za binadamu ni nukta muhimu ambazo Uturuki inapaswa kuzingatia katika hatua zake nchini Syria.