Ankara yaziambia nchi za Kiarabu: Msiingie katika mchezo wa Israel
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i137638-ankara_yaziambia_nchi_za_kiarabu_msiingie_katika_mchezo_wa_israel
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki amezihutubu nchi za Kiislamu na kuzitahadharisha ziwe makini na kutoingia katika mchezo wa utawala wa Kizayuni Israel.
(last modified 2026-03-28T04:42:59+00:00 )
Mar 28, 2026 04:42 UTC
  • Hakan Fidan
    Hakan Fidan

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki amezihutubu nchi za Kiislamu na kuzitahadharisha ziwe makini na kutoingia katika mchezo wa utawala wa Kizayuni Israel.

Hakan Fidan amesema: Nchi za eneo la Ghuba ya Uajemi hazipasi kujiiingiza katika mchezo wa Israel. Fidan ameutaja utawala wa kizayuni kuwa ni kikwazo kikuu katika kufikiwa amani na kuongeza kuwa: Ukosefu wa amani katika eneo hilo unasababisha mapigano ya muda mrefu kati ya nchi na jamii mbalimbali. 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki ameashiria kupungua imani ya Tehran kwa Washington na kusema, Iran kwa kiasi kikubwa haiiamini Marekani.

Wakati huo huo Ahmet Hakan, Mhariri Mkuu wa gazeti la Hurriyet la nchini Uturuki ameandika katika makala kwamba: Rais Donald Trump wa Marekani alikuwa na ndoto nyingi kuhusu vita; Alitaka kuiangusha serikali ya Iran lakini hakuweza. 

"Alitaka kuilazimisha Iran isalimu amri, ameshindwa. Alitaka kudhibiti mafuta ya Iran, ameshindwa. Alitaka kuwaingiza watu wake madarakani ameshindwa.  Alitaka kuifanya Iran kama Venezuela lakini ameshindwa, amesema Mhariri Mkuu wa Hurriyet. 

Amesema kuwa: "Ukweli mchungu umevunja ndoto hizo zote. Mwishowe, ndoto moja tu imebaki kwa Trump: Kufungua Lango Bahari la Hormuz. Yaani, anatarajia kutangaza ushindi kwa kufungua Lango Bahari la Hormuz, ambalo lilikuwa wazi kabla ya vita."