Maroketi ya Yemen yasambaratisha kambi ya jeshi ya Saudia, Najran
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i44422-maroketi_ya_yemen_yasambaratisha_kambi_ya_jeshi_ya_saudia_najran
Vikosi vya Jeshi la Yemen vimevurumisha maroketi katika kambi moja ya kijeshi ya Saudi Arabia katika mkoa wa kusini wa Najran, na kuharibu silaha nyingine kikiwemo kifaru cha kijeshi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 13, 2018 03:27 UTC
  • Maroketi ya Yemen yasambaratisha kambi ya jeshi ya Saudia, Najran

Vikosi vya Jeshi la Yemen vimevurumisha maroketi katika kambi moja ya kijeshi ya Saudi Arabia katika mkoa wa kusini wa Najran, na kuharibu silaha nyingine kikiwemo kifaru cha kijeshi.

Shirika la habari la Saba limetangaza habari hiyo na kuongeza kuwa, katika muendelezo wa hujuma za kulipiza kisasi, Jeshi la Yemen limevurumisha maroketi dhidi ya kituo cha kijeshi cha al-Talah mkoani Najran, na kuharibu silaha za utawala wa Aal-Saudi kikiwemo kifaru.

Hata hivyo shirika hilo halijatoa maelezo zaidi kuhusu shambulizi hilo.

Siku chache zilizopita, wanajeshi wa Yemen walitumia makombora yaliyoundwa nchini humo kushambulia maeneo kadhaa ya kijeshi na kiuchumi ya Saudia Arabia ukiwemo mji mkuu wa nchi hiyo, Riyadh.

Roketi  la Yemen likivurumishwa

Mashambulizi hayo yote ni katika oparesheni za kulipiza kisasi jinai za Saudia dhidi ya raia wa Yemen.

Ikumbukwe kuwa Saudia ilianzisha hujuma yake dhidi ya Yemen mnamo Machi mwaka 2015 kwa lengo la kuirejesha madarakani serikali kibaraka ya Abdu Rabuh Mansour Hadi aliyejiuzulu urais na kukimbilia mji mkuu wa Saudia, Riyadh, ambapo watu zaidi ya 14,000 wameuawa na mamilioni ya wengine kujeruhiwa.