Dec 06, 2018 08:00 UTC
  • Utawala wa Aal Khalifa Bahrain washindwa kuhalalisha mamlaka yake

Mkuu wa Jumuiya ya Haki za Binadamu na Demokrasia ya Bahrain amesema kuwa, jitihada za utawala wa Aal Khalifa za kuuhalalisha utawala huo kupitia ushiriki wa wananchi kwenye uchaguzi zimegonga mwamba.

Duru ya kwanza ya uchaguzi wa Bunge na mabaraza ya miji Bahrain ilifanyika tarehe 24 mwezi Novemba na duru ya pili ilifanyika  Disemba Mosi nchini humo ambapo wananchi, makundi na vyama mbalimbali vimesusia uchaguzi huo wa kimaonyesho. 

Abdul ilah  al Mahuzi Mkuu wa Jumuiya ya Haki za Binadamu na Demokrasia ya Bahrain ameashiria namna uchaguzi wa Bunge wa nchi hiyo ulivyokuwa na sura ya kidikteta badala ya kuwa wa kidemokrasia na akasema, kiwango cha ushiriki wa wananchi katika uchaguzi huo kilikuwa cha chini. Amesema kitendo cha kuwalazimisha watu kupiga kura kwenye uchaguzi huo wa kimaonyesho ambao umeingia katika duru ya pili, kinaonyesha namna Bahrain inavyokabiliwa na mgogoro mkubwa wa kisiasa. 

Abdul ilah al Mahuzi ameashiria pia tabia ya utawala wa Aal Khalifa ya kutoheshimu haki za binadamu na kupuuza taasisi za kimataifa na kueleza kuwa: Kuendelea kutolewa hukumu za kunyongwa wafungwa wasio na hatia, kuendelea kufutwa uraia wa wananchi, utiaji mbaroni na pia kupuuzwa haki za kisiasa za raia wa Bahrain kupitia vitisho na hofu ili wasalimu amri mbele ya matakwa ya utawala ulioko madarakani, yote hayo yanaonyesha kushtadi ukiukaji wa haki za binadamu  nchini Bahrain.  

Wafungwa wa Bahrain na mateso wanayokabiliana nayo

 

Tags