Jun 15, 2023 11:47 UTC
  • Utawala wa Aal Khalifa waendelea kuwakamata vijana wa Bahrain

Utawala wa Aal Khalifa nchini Bahrain unaendelea kuwakamata kiholela vijana wa kiume na kike wa nchi hiyo katika maeneo tofauti ya nchi kwa sababu za kisiasa.

Tangu Februari 14, 2011, Bahrain imekuwa uwanja wa harakati za mapinduzi ya wananchi dhidi ya utawala wa Aal-Khalifa, na katika kipindi hicho, zaidi ya raia 15,000 wa Bahrain wametiwa mbaroni kwa tuhuma za uongo, na idadi kubwa ya wapinzani kupokonywa uraia wao.

Mtandao wa ufuatiliaji wa mashambulizi nchini Bahrain umetangaza kuwa utawala wa Aal-Khalifa hici karibuni umekamata na kumshikilia kizuizini Hussein Ayoub, kijana wa Bahrain, kutoka mji wa Abu Quwa.

Awali, Yousef Ghalib kutoka mkoa wa Aali alikamatwa katika shambulio lililofanywa na vikosi vya usalama vya Aal Khalifa katika eneo la  Karzkan.

Idadi ya vijana wa Bahrain waliokamatwa kiholela na utawala huo imeongezeka hadi vijana watano 5 katika nusu ya kwanza ya mwezi huu wa Juni.

Kukamatwa vijana hao kunakuja wakati idadi ndogo ya wafungwa wanaokaribia kumaliza vifungo vyao wakiachiliwa na kutumikia kifungo kilichosalia gerezani kama sehemu ya kile kinachoitwa vifungo mbadala.

Utawala wa Bahrain umekamata idadi kubwa ya raia wake ili kuzima maandamano ya wananchi dhidi yake. Licha ya hatua zote hio za utawala wa Aal-Khalifa, lakini harakati za mapinduzi ya wananchi zingali zinaendelea kwa ajili ya kutekelezwa matakwa yao halali na ya kisheria.

Tags