Harakati ya Hizbullah: Marekani inaondoka Syria kutokana na kushindwa
Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, Marekani inaondoka nchini Syria kutokana na kushindwa siasa zake katika Mashariki ya Kati na kutoweza kuuhami na kuulinda utawala haramu wa Israel.
Sheikh Naim Qassim amesema hayo kusini mwa Beirut mji mkuu wa Lebanon katika shughuli ya kumbukumbu ya mwaka wa tatu wa kuuawa shahidi Samir al-Kuntar ambapo ameashiria tangazo la Marekani la kuondoa majeshi yake nchini Syria baaya ya kusambaratishwa kikamlifu kundi la Daesh na kusema bayana kwamba, maneno hayo ni kioja nakichekesho kwani, Wamarekani wenyewe ndio waliolianzisha kundi hilo la kigaidi na kwa hatua yao ya kulipatia silaha wakawa wamesaidia kurefusha umri wa magaidi hao.
Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesisitiza kuwa, utawala ghasibu wa Israel ndio chanzo na chimbuko la migogoro yote ya Mashariki ya Kati na kuongeza kuwa, utawala wa Tel-Aviv umewafanya Wapalestina kuwa wakimbizi na kuyakalia kwa mabavu baadhi ya maeneo ya nchi za Kiarabu ya misri, Syria, Jordan na Lebanon.

Kiongozi huyo mwandamizi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amebainisha kwamba, utawala dhalimu wa Israel daima umekuuwa ukiendesha njama na fitina katika eneo hili.
Sheikh Naim Qassim amesisitiza kuwa, hakuna njia yoyote ile ya kuukabiliana na utawala vamizi wa Israel bighairi ya muqawama na mapambano na kwamba, mwenendo wa mapatano katu hauwezi kuipatia ufumbuzi kadhia ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu na Wazayuni maghasibu.