Saudia yatishia kuwaadhibu raia wake waliokwenda Russia na kukataa kurudi nyumbani
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i50473-saudia_yatishia_kuwaadhibu_raia_wake_waliokwenda_russia_na_kukataa_kurudi_nyumbani
Ubalozi wa Saudia mjini Moscow umetishia kuwa, Riyadh itawaadhibu vikali raia wa nchi hiyo waliokwenda kwenye mashindano ya fainali za kombe la dunia la mpira wa miguu nchini Russia na hadi hivi sasa wanang'ang'ania kubakia huko huko hawataki kurudi nchini Saudi Arabia.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 28, 2018 03:31 UTC
  • Saudia yatishia kuwaadhibu raia wake waliokwenda Russia na kukataa kurudi nyumbani

Ubalozi wa Saudia mjini Moscow umetishia kuwa, Riyadh itawaadhibu vikali raia wa nchi hiyo waliokwenda kwenye mashindano ya fainali za kombe la dunia la mpira wa miguu nchini Russia na hadi hivi sasa wanang'ang'ania kubakia huko huko hawataki kurudi nchini Saudi Arabia.

Ubalozi huo umetoa vitisho hivyo kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter na kusema kuwa raia wa nchi hiyo waliokwenda Russia kwa ajili ya kuishabikia timu ya nchi yao na ambao wamagoma kurudi Saudi Arabia wana muda wa hadi tarehe 31 mwezi huu wa Disemba wahakikishe wameondoka Russia na kurejea kwao kabla ya hatua kali hazijachukuliwa dhidi yao.

Vitisho hivyo vimetolewa na ubalozi wa Saudi Arabia mjini Moscow katika hali ambayo raia hao wa Saudia wanaishi kihalali huko Russia kwa vibali kamili kutoka kwa mamlaka husika za Russia.

Dunia bado inauguza majeraha ya ukatili na unyama aliofanyiwa Jamal Khashoggi katika ubalozi mdogo wa Saudia mjini Istanbul, Uturuki na tayari ubalozi wa nchi hiyo Moscow unatoa vitisho vingine dhidi ya raia wa Saudi Arabia wanaoishi kihalali nchini Russia

Wanaharakati wa haki za binadamu wanasema kuwa, balozi za Saudi Arabia katika nchi za kigeni badala ya kuwalinda na kuwahudumia raia wa nchi hiyo, zinafanya kazi za kutoa vitisho na mauaji dhidi yao.

Watumiaji wa mitandao ya kijamii wamessema kuwa, tishio hilo la ubalozi wa Saudi Arabia mjini Moscow Russia ni sawa na mauaji yaliyofanywa na maafisa wa Saudia katika ubalozi mdogo wa nchi hiyo wa mjini Istanbul Uturuki dhidi ya mwandishi Jamal Khashoggi raia wa Saudi Arabia ambaye baada ya kukataa kurudi nchini humo aliuliwa kinyama, kukatwakatwa viungo vyake na hadi hivi sasa mwili wake haujulikani ulipo.

Shirika la Kijasusi la Marekani CIA limesema kuwa, kwa mujibu wa ushahidi lilio nao, Mohammed bin Salman, mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudi Arabia ndiye aliyetoa amri ya kuuliwa kinyama Khashoggi.