UN yatahadharisha kuhusu hali mbaya inayowakabili wakimbizi wa Syria
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i51727-un_yatahadharisha_kuhusu_hali_mbaya_inayowakabili_wakimbizi_wa_syria
Umoja wa Mataifa umetahadharisha kuhusu hali ya kutisha waliyonayo wakimbizi walioukimbia mji wa Hajin huko mashariki mwa Syria kutokana na mashambulizi ya kundi la kigaidi la Daesh.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Feb 22, 2019 13:16 UTC
  • UN yatahadharisha kuhusu hali mbaya inayowakabili wakimbizi wa Syria

Umoja wa Mataifa umetahadharisha kuhusu hali ya kutisha waliyonayo wakimbizi walioukimbia mji wa Hajin huko mashariki mwa Syria kutokana na mashambulizi ya kundi la kigaidi la Daesh.

Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Stephane Dujarric ametoa wito wa kulindwa wakimbizi wa Syria ambao wanakabiliwa na hatari ya kifo kutokana na baridi kali na ukosefu wa chakula. Dujarric amesema kuwa, wakimbizi waliko kaskazini mwa Syria wanazingirwa katika eneo linalodhibitiwa na kundi la kigaidi la Daesh na hawapati misaada wala huduma zozote za afya. Amesema kuna udharura wa kuhakikisha kuwa, wakimbizi hao wanapata misaada na huduma mbalimbali zikiwemo za afya. 

Magaidi wa Daesh katika mji wa Hajin, Syria

Imeelezwa kuwa, baadhi ya raia hao wamefika katika kambi za wakimbizi wakiwa na  hali mbaya. Ripoti zinasema kuwa watoto 61 wakimbizi wa Syria wameaga dunia wakiwa njiani kuelekea katika kambi ya wakimbizi ya Al Hawl wakitokea katika mji wa Hajin. Kambi hiyo ina jumla ya wakimbizi elfu 41.