HAMAS: Taifa la Palestina limethibitisha kwamba, Masjidul Aqswa ni mstari mwekundu
(last modified Sat, 23 Feb 2019 07:32:51 GMT )
Feb 23, 2019 07:32 UTC
  • HAMAS: Taifa la Palestina limethibitisha kwamba, Masjidul Aqswa ni mstari mwekundu

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imetangaza kuwa, msikiti wa al-Aqswa ni mstari mwekundu wa Umma wa Kiislamu.

Taarifa iliyotolewa jana na Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS sambamba na maandamano ya mamia ya maelfu ya Wapalestina katika mji wa Quds imeeleza kwamba, utawala haramu wa Israel katu hautafanikiwa kubadilisha ukweli kuhusiana na msikiti huo mtakatifu.

Harakati ya Hamas imeyataka pia mataifa ya Kiarabu na Kiislamu kusimama kidete na kukabiliana na njama za utawala vamizi wav Israel za kuyayahudisha maeneo ya Waislamu huko Palestina.

Kadhalika Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imewataka Waislamu kote ulimwenguni kujitokeza na kuuhami mji wa Baytul-Muqaddas mkabala na njama za adui Mzayuni.

Ismail Hania, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS

Itakumbwa kuuwa, juzi makundi ya muqawama na mapambano ya Palestina yalitoa onyo kwa utawala ghasibu wa Kizayuni kutokana na kuendelea kuuvunjia heshima msikiti mtakatifu wa al-Aqswa, kibla cha kwanza cha Waislamu.

Katika taarifa yao hiyo, makundi ya muqawama ya Palestina yalisisitiza pia kwamba, Uchokozi na uvamizi huo wa utawala haramu wa Kizayuni unafanyika mbele ya kimya cha nchi za Kiarabu na Kiislamu na ushindani wa wazi wazi wa baadhi ya watawala wa Kiarabu wa kugombania kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Hali katika msikiti wa Al Aqsa imekuwa tete na ya taharuki kufuatia hatua ya hivi karibuni ya utawala wa Kizayuni ya Israel kuwafungia Waislamu Wapalestina Babu-Rahmah, moja ya milango ya kuingilia msikiti huo mtukufu.

Tags