Syria: Hatutosita kukabiliana na ukaliwaji mabavu wa milima yetu ya Golan
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i51984-syria_hatutosita_kukabiliana_na_ukaliwaji_mabavu_wa_milima_yetu_ya_golan
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria, Faisal Mekdad amesisitiza kwamba, serikali ya Damascus haitosita kukabiliana na njama za utawala haramu wa Israel zenye lengo la kuendelea kuikalia kwa mabavu milima ya Golan.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 06, 2019 10:42 UTC
  • Syria: Hatutosita kukabiliana na ukaliwaji mabavu wa milima yetu ya Golan

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria, Faisal Mekdad amesisitiza kwamba, serikali ya Damascus haitosita kukabiliana na njama za utawala haramu wa Israel zenye lengo la kuendelea kuikalia kwa mabavu milima ya Golan.

Mekdad ameyasema hayo alipokutana na Christian Lund, Mkuu wa Kamati ya Kulinda Amani ya Umoja wa Mataifa pamoja na ujumbe aliouongoza mjini Damascus, ambapo sambamba na kusisitiza udharura wa kukomeshwa ukiukaji wa maazimio ya Umoja wa Mataifa na kadhalika uungaji mkono kwa makundi ya kigaidi unaofanywa na utawala huo wa Kizayuni, amesema kuwa, vitendo hivyo vya Tel Aviv vinatishia usalama na amani ya kimataifa. 

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria, Faisal Mekdad

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria, Faisal Mekdad ameashiria mwendelezo wa mapambano ya nchi yake dhidi ya makundi ya kigaidi na kubainisha kwamba, kipaumbele cha serikali ya Damascus ni kurejesha usalama na uthabiti ndani ya nchi yote na kupatikana suluhu ya kiuadilifu sambamba na kuieneza katika eneo lote la Mashariki ya Kati. Hivi karibuni pia na akizungumza na Marcelo Montaner, Mkuu wa Majeshi ya Uruguay aliyetembelea Syria, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria, alisema kuwa kukombolewa na kudhibitiwa upya milima ya Golan inayokaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni ni haki ya kisheria ya serikali na taifa la Syria. Miinuko hiyo ilikaliwa kwa mabavu na utawala haramu wa Kizayuni mwaka 1967 katika Vita vya Siku Sita vya utawala huo vamizi na nchi za Kiarabu, hata hivyo tangu wakati huo jamii ya kimataifa imekataa kuitambua miinuko hiyo kuwa sehemu ya Israel.