Gaidi mmoja Mmarekani auawa kaskazini mwa Iraq
(last modified Sun, 21 Apr 2019 06:39:00 GMT )
Apr 21, 2019 06:39 UTC
  • Gaidi mmoja Mmarekani auawa kaskazini mwa Iraq

Duru za habari zimeripoti kuwa mwanajeshi mmoja gaidi wa Marekani ameuawa kaskazini mwa Iraq.

Kwa mujibu wa shirika la habari la FARS, taarifa iliotolewa na muungano unaodaiwa ni wa kupambana na magaidi wa Daesh unaoongozwa na Marekani nchini Iraq imesema kuwa, gaidi huyo wa Kimarekani aliuawa jana Jumamosi katika mkoa wa Nainawa (Nineveh) wa kaskazini mwa Iraq akiwa katika operesheni maalumu.

Mwaka 2011 jeshi la Marekani lilitangaza kuondoa wanajeshi wake nchini Iraq baada ya kuikalia kwa mabavu nchi hiyo kwa muda wa miaka minane.

Magaidi wakufurishaji wa ISIS waliozushwa na Marekani na kupewa mafunzo, silaha na fedha ili kufanya jinai katikanchi za Iraq na Syria.

 

Hata hivyo mwaka 2014 nchi hiyo ya kibeberu ilirejesha wanajeshi wake nchini humo kwa madai ya kupambana na magaidi wa Daesh (ISIS). 

Hivi sasa Marekani ina kambi kadhaa za kijeshi nchini Iraq na kwa mujibu wa Donald Trump, Marekani haina nia kabisa ya kuondoa wanajeshi wake nchini humo licha ya malalamiko na upinzani mkubwa wa Wairaq wanaotaka wanajeshi hao vamizi waondoke haraka nchini mwao hasa kwa kuzingatia kuwa madai ya kuweko kwao huko hayapo tena baada ya kusambaratishwa kikamilifu magaidi wa ISIS nchini Iraq.

Tags