Aug 10, 2019 07:40 UTC
  • Yemen yawakamata mamluki waliomuua Ibrahim al Houthi

Idara za intelijensia nchini Yemen zimefanikiwa kuwakamata mamluki waliomuua Ibrahim Badreddin al Houthi, kaka yake Katibu Mkuu wa Harakati ya Ansarullah.

Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Serikali ya Uokovu wa Kitaifa Yemen, mamluki wanaofungamana na wavamizi Wasaudi, Wamarekani na Wazayuni, siku ya Ijumaa walimpiga risasi na kumuua Sayyid Ibrahim Badreddin al Houthi, kaka yake, Sayyid Abdul Malik Badreddin al Houthi, Katibu Mkuu wa Harakati ya Ansarullah.

Kwa mujibu wa taarifa ya Televisheni ya Al Mayadeen, idara za upelelezi nchini Yemen zimefanikiwa kuwakamata waliomuua Ibrahim al Houthi na pia wakati huo huo kuwakamata magaidi kadhaa katika oparesheni hiyo.

Sayyid Abdul Malik Badreddin al Houthi, Katibu Mkuu wa Harakati ya Ansarullah

Taarifa zinadokeza kuwa waliomuua Ibrahim al Houthi wanafungamana na wizara ya ujasusi ya Saudia na katika mauaji hayo, walielekezwa na kinara wa wanamgamabo wa utawala wa Ali Abdullah Saleh, dikteta wa zamani Yemen aliyetimuliwa madarakani.

Tags