Dec 09, 2019 08:11 UTC
  • Israel imewakamata Waplestina milioni moja tokea ikalie ardhi zao kwa mabavu

Taasisi moja ya takwimu Palestina imetangaza kuwa, tokea utawala haramu wa Israel ukalie kwa mabavu ardhi za Palestina mwaka 1948 hadi sasa, Wapalestina wapatao milioni moja wamekamatwa kwa sababu mbali mbali.

Aidha takwimu hizo zinaonyesha kuwa tokea Intifadha ya Kwanza ya Palestina ianze mwaka 1987 hadi sasa, Israel imewakamata Wapalestina 343,000.

Riyadh Al Ashqar, Msemaji wa Taasisi ya Utafiti wa Mateka Wapalestina amesema: "Pamoja na kuwepo ongezeko la Wapalestina wanaokamatwa na wanajeshi wa utawala wa Kizayuni lakini utawala huo haujaweza kufikia malengo yake ya kuwafanya Wapalestina wasalimu amri." Aidha amesema Wapalestina wataendeleza mapambano yao hadi pale ardhi zao zitakapokombolewa.

Riyadh al Ashqar, ameendelea kusema kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel unawakamata Wapalestina kiholela  ili kujaribu kuvunja azma yao  na mbinu hiyo ingali inaendelea.

Askari wa utawala wa Kizayuni wa Israel wakimtia mbaroni mtoto mdogo

Hivi sasa kuna Wapalestina 57,000 wanaoshikiliwa katika magereza ya utawala wa Kizayuni wa Israel ambapo 250 miongoni mwao ni wanawake na 47 ni watoto.

Wafungwa hao wa Kipalestina wamekuwa wakilalamika kuwa wanateswa na kudhalilishwa katika magereza hayo ya kuogofya ya utawala katili wa Israel.

Tags