Wanajeshi wa Sudan waendelea kuondoka nchini Yemen
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i57912-wanajeshi_wa_sudan_waendelea_kuondoka_nchini_yemen
Vyombo vya habari vimeripoti kuwa, wanajeshi wengine wa Sudan waliokuwa wametumwa kuivamia Yemen, wameondoka nchini humo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 16, 2019 04:16 UTC
  • Wanajeshi wa Sudan waendelea kuondoka nchini Yemen

Vyombo vya habari vimeripoti kuwa, wanajeshi wengine wa Sudan waliokuwa wametumwa kuivamia Yemen, wameondoka nchini humo.

Televisheni ya al Mayadeen imeripoti kuwa, vikosi vinne vya jeshi la Sudan vimeondoka katika eneo linalojulikana kwa jina la Ufukwe wa Magharibi huko Yemen na hivi sasa vimebakia vikosi viwili tu vya nchi hiyo katika eneo hilo. 

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Wasudan wamepunguza idadi kubwa ya wanajeshi wao huko Yemen ingawa hawajawaondoka wote.

Katika upande mwingine, vyombo vya usalama vya Yemen katika mikoa ya Raymah, Dhamar, San'a, al Hudaidah, Hajjah, Ibb na 'Amran zimetangaza kuwa, katika nusu ya kwanza ya mwezi huu wa Disemba, mamluki 162 wamejitenga na muungano vamizi unaoongozwa na Saudi Arabia.

Wanajeshi wa Sudan wakiwasili Yemen kwa amri ya Omar al Bashir

 

Baada ya Saudi Arabia kuunda muungano vamizi na kuanzisha mashambulizi makali ya kikatili dhidi ya nchi maskini ya Yemen mwezi Machi 2015, maelfu ya mamluki wa Sudan waliingia Yemen kufanya jinai dhidi ya Waislamu wa nchi hiyo. Hata hivyo mamluki wengi nao wameangamizwa na wanamapambano shupavu wa Yemen.

Matunda ya uvamizi huo wa Saudia na kundi lake dhidi ya nchi hiyo maskini ya Kiarabu ni kuuliwa bila hatia maelfu ya raia, kuvurugwa miunduombinu ya Yemen na hasara nyingine nyingi za roho na mali za umma. Hata hivyo muqawama wa kishujaa wa wananchi, jeshi na kamati za kujitolea za wananchi wa Yemen umewakwamisha wavamizi hao kufikia malengo yao haramu.