Jeshi la Yemen laendelea kupata ushindi katika mkoa wa al Jawf
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i59829-jeshi_la_yemen_laendelea_kupata_ushindi_katika_mkoa_wa_al_jawf
Miji mingi katika mkoa wa al Jawf ulioko kaskazini mwa Yemen imekombolewa kutoka mikononi mwa mamluki wa Saudi Arabia baada ya mapigano makali yaliyojiri kati ya jeshi la nchi hiyo linaloshirikiana na makundi ya kujitolea ya wananchi na mamkuki wa Saudi Arabia.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 18, 2020 23:14 UTC
  • Jeshi la Yemen laendelea kupata ushindi katika mkoa wa al Jawf

Miji mingi katika mkoa wa al Jawf ulioko kaskazini mwa Yemen imekombolewa kutoka mikononi mwa mamluki wa Saudi Arabia baada ya mapigano makali yaliyojiri kati ya jeshi la nchi hiyo linaloshirikiana na makundi ya kujitolea ya wananchi na mamkuki wa Saudi Arabia.

Brigedia Jenerali Yahya Sare'e Msemaji wa jeshi la Yemen jana alitangaza kuwa, jeshi la nchi hiyo linafanya juhudi kubwa za kuhakikisha kwamba mkoa huo unarejea katika hali ya kawaida. 

Jeshi la Yemen aidha limesisitiza kuwa askari jeshi wa kikosi cha sita wa jeshi hilo limewafurisha kikamilifu mamluki wa Saudia katika mkoa wa al Jawf na kuwauwa mamia ya wengine miongoni mwao. Katika mapigano hayo jeshi la Yemen pia limewakamata mateka mamluki kadhaa. 

Mamluki wa Saudi Arabia waliotiwa mbaroni na jeshi la Yemen 

Jeshi la Yemen limesisitiza kuwa ushindi wa jeshi hilo utaendelea hadi kukombolewa kikamilifu ardhi ya Yemen.  

Katika upande mwingine ndege za kivita za Saudi Arabia jana Jumatano zilikishambulia mara mbili kijiji cha Saruah huko magharibi mwa mkoa wa Marib. Televisheni ya al Masirah imetangaza kuwa wanajeshi vamizi wa Saudi Arabia wameushambulia mji ulio chini ya mzingiro wa al Duraihim mkoani  al Hudaiydah.