Jul 27, 2020 07:24 UTC
  • Wapalestina 27 wauawa shahidi miezi sita ya kwanza mwaka 2020

Wapalestina 27 wameuawa shahidi kwa kupigwa risasi na wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel katika nusu ya kwanza ya mwaka huu wa 2020.

Kwa mujibu wa Kituo cha Takwimu cha Palestina,  kinachofungamana na Harakati ya Ukombozi wa Palestina (PLO) , katika miezi sita ya kwanza ya mwaka 2020, Wapalestina 27 wakiwemo watoto saba na wanawake wawili waliuawa shahidi kwa kupigwa risasi na wanajeshi wa utawala haramu wa Israel huku wengine 70 wakijeruhiwa.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, katika miezi sita ya kwanza ya mwaka huu, Wapalestina 2,330 walikamatwa na miongoni mwao 304 na wengine 70 walitekwa nyara.

Ripoti hiyo imeongeza kuwa, utawala wa Kizayuni katika miezi sita ya kwanza ya mwaka huu uliharibu nyumba 357 za Wapalestina na aghalabu ya nyumba hizo zilikuwa katika maeneo ya Al Khalil na Quds Tukufu (Jerusalem) inayokaliwa kwa mabavu.

Mazishi ya Mpalestina aliyeuawa shahidi kwa kupigwa risasi na wanajeshi wa utawala haramu wa Israel

Utawala wa Kizayuni aidha katika muda huu uliidhinisha ujenzi wa karibu nyuma 15,000 za walowezi wa Kizayuni katika ardhi za Wapalestina zilizoporwa.

Hali kadhalika katika miezi sita ya kwanza ya mwaka huu, jumla ya walowezi wa Kizayuni na Makuhani 10,000 waliuvamia na kuuvunjia heshima Msikiti wa Al Aqsa kwa himaya ya utawala wa Kizayuni. 

Tags