Maandamano dhidi ya Benjamin Netanyahu yaendelea kushuhudiwa
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i63551-maandamano_dhidi_ya_benjamin_netanyahu_yaendelea_kushuhudiwa
Maelfu ya wakazi wa Palestina inayokaliwa kwa mabavu (Israel) usiku wa jana walifanya maandamano makubwa na kukusanyika mbele ya makao ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu na kutoa wito wa kujizulu kiongozi huyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 21, 2020 04:35 UTC
  • Maandamano dhidi ya Benjamin Netanyahu yaendelea kushuhudiwa

Maelfu ya wakazi wa Palestina inayokaliwa kwa mabavu (Israel) usiku wa jana walifanya maandamano makubwa na kukusanyika mbele ya makao ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu na kutoa wito wa kujizulu kiongozi huyo.

Waandamanaji hao wenye hasira huku wakiwa wamebeba mabango na maberamu walisika wakipiga nara dhidi ya Benjamin Netanyahu na kumtaka ajiuzulu wadhifa wake huo na kujitenga kabisa na siasa kutokana kukabiliwa na tuhuma lukuki za ufisadi.

Katika miezi ya hivi karibuni Israel imekuwa ikishuhudia maandamano makubwa ambayo yanamtaka Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu ajiuzulu kutokana na kile wanachosema waandamanaji kwamba, kushindwa kwake kukabiliana na changamoto zinazowakabili.

Maandamano hayo yanafanyika kila Jumapili na kuhudhuriwa na maelfu ya watu. Netanyahu na baraza lake la mawaziri wanalaumiwa kwamba, badala ya kutanguliza mbele matatizo ya kiafya na kiuchumi yanayoisumbua Israel kwa sasa, wameng’ang’ania kusukuma mbele gurudumu la mipango ya kuzikalia kwa mabavu ardhi za Palestina. 

Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Israel

 

Baadhi ya duru za Israel zimeripoti kuwa, chama cha Blu na Nyeupe cha Benny Gantz ambacho kinahesabiwa kuwa muitifaki wa Netanyahu katika kuunda serikali na ambaye ni Waziri wa Vita kimetangaza kuunga mkono maandamano hayo yaliyo dhidi ya Netanyahu, msimamo ambao unaonesha ni kwa jinsi gani serikali ya Waziri Mkuu wa Israel inakabiliwa na mgawanyiko.