Oct 06, 2020 07:26 UTC
  • Russia yatahadharisha kuhusu hatua mbaya za Marekani huko Syria

Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Russia ametahadharisha kuhusu maafa ya mienendo ya Marekani na Wakurdi wa Syria na kusisitiza ulazima wa kuzuia hatua yoyote inayotaka kuigawa ardhi ya nchi hiyo.

Sergey Lavrov ametahadharisha kuhusu matokeo mabaya ya hatua ya Marekani ya kuwachochea Wakurdi wa Syria dhidi ya serikali ya nchi hiyo kwa ajili ya kuanzisha utawala wao kaskazini mwa Syria na kusema: Hatari hiyo itakuwa na madhara kwa kanda ya maghribi mwa Asia, Ulaya na hata Russia.

Lavrov ameongeza kuwa Wakurdi wapo katika nchi kadhaa za magharibi mwa Asia na wito wa kujitenga kaumu hiyo utakuwa na madhara mkubwa. 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia ameashiria mapambano dhidi ya ugaidi na kusema kuwa, Damascus imekuwa ikisisitiza kuwa wanamgambo wa Kikurdi na makundi ya magaidi yanayofadhiliwa na Marekani huko mashariki na kaskazini mwa Syria hayana lengo jingine ghairi ya kupora mafuta ya nchi hiyo.

Wamarekani wanashirikiana na Wakurdi wa Syria kuiba mafuta ya nchi hiyo

Ripoti rasmi zinaonyesha kuwa hadi sasa Marekani imeyapa makundi ya kigaidi nchini Syria silaha na zana za kijeshi zenye thamani ya mabilioni ya dola. 

Marekani imetuma majeshi yake kaskazini mwa Syria na kuikalia kwa mabavu sehemu hiyo.    

Tags