Wapalestina waandamana, wataka kuachiwa huru Maher al Akhras
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i64361-wapalestina_waandamana_wataka_kuachiwa_huru_maher_al_akhras
Wananchi wa Palestina wamefanya maandamano leo wakitangaza uungaji kono wao kwa matekani Mpalestina anayeshikiliwa katika korokoro ya utawala haramu wa Israel, Maher al Akhras.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Nov 01, 2020 04:37 UTC
  • Maher al Akhras
    Maher al Akhras

Wananchi wa Palestina wamefanya maandamano leo wakitangaza uungaji kono wao kwa matekani Mpalestina anayeshikiliwa katika korokoro ya utawala haramu wa Israel, Maher al Akhras.

Waandamanaji hao wametoa wito wa kuachiwa huru mara moja mateka huyo ambaye anafanya mgomo wa kula kwa karibu siku mia moja zilizopita. 

Waandamanaji hao pia wametoa nara zinazoulaani utawala haramu wa Israel na hatua yake ya kuendelea kumshikilia Maher al Akhras licha ya hali yake mbaya ya kiafya.

Mkuu wa Tume ya Masuala ya Mateka wa Palestina Qadri Abubakr amesema kuwa Maher al Akhras amepoteza uwezo wake wa kuona na kusikia kutokana na mgomo wa kula akipinga unyanyasaji wa utawala haramu wa Israel.

Siku chache zilizopita pia ripota wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu zilizopewa jina la Israel aliutaka utawala wa Kizayuni umwachie Mpalestina Maher al Akhras haraka iwezekanavyo.

Kwa mujibu wa gazeti la Al-Qudsul-Araby, Michael Lynk, ripota wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Israel  amesema kuwaweka kizuizini Wapalestina ni ukiukaji wa wazi wa Makubaliano ya Nne ya Geneva na akasisitiza kuwa Israel inapaswa iyaheshimu makubaliano hayo.

Mateka wa Palestina katika korokoro za Israel

Maher al Akhras, Mpalestina mwenye umri wa miaka 49, mkazi wa mji wa Jenin katika eneo la Ufukwe wa Magharibi wa Mto Jordan alikamatwa tarehe 27 Julai na kuwekwa kizuizini bila kuelezwa anakabiliwa na mashtaka gani.

Karibu mateka 4,800 wa Palestina wakiwemo wanawake 41 na watoto 140 wanashikiliwa katika jela za kuogofya za utawala wa Kizayuni wa Israel. Mateka hao wa Palestina ni miongoni mwa waathirika wakubwa wa jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel.