Dec 18, 2020 12:01 UTC
  • Jordan yasisitiza kuiunga mkono Quds na Palestina

Mfalme wa Jordan amesisitiza kuiunga mkono nchi huru ya Palestina ambayo mji wake mkuu utakuwa Quds Tukufu.

Mfalme Abdallah wa Pili wa Jordan amesema kuwa, Jordan inawaunga mkono ndugu zao Wapalestina na inaendelea kuwasiliana na pande za kimataifa kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wa Palestina. Mfalme wa Jordan ameongeza kuwa amani ya kiadilifu na ya muda mrefu itapatikana kwa mdingi wa serikali mbili kama chaguo la kistratejia na litakalodhamini kuundwa nchi huru ya Palestina mji wake mkuu ukiwa Quds. 

Akihutubia hivi karibuni Mfalme wa Jordan amebainisha kuwa uangalizi wa Jordan kwa maeneo matukufu ya Kiislamu na Kikristio ni wajibu na jukumu ambalo wanajivunia tangu zaidi ya miaka 100 iliyopita. 

Wizara ya Masuala ya Wakfu na Kidini ya Jordan ndiyo inayosimamia maeneo matukufu ya Kiislamu katika mji wa Quds huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu tangu mwaka 1948 hadi sasa. Msikiti wa al Aqsa ambao ni nembo kuu ya utambulisho wa Kiislamu na Palestina katika mji wa Baitul Muqaddas mara kwa mara umekuwa ukikabiliwa na hujuma na uvamizi wa utawala wa Kizayuni unaoikalia Quds kwa mabavu. 

Msikiti wa al Aqsa, nembo kuu ya utambulisho wa Waislamu 

 

Tags