Chinjachinja wa Daesh atiwa mbaroni huko Talafar, Iraq
Idara ya Intelijinisia ya jeshi la Iraq imetangaza habari ya kutiwa mbaroni kinara mashuhuri wa magaidiwa kundi la kitakfiri la Daesh anayefahamika kwa jina la Cihnjachinja huko Talafar nchini humo.
Idara ya Intelijinisia ya jeshi la Iraq jana ilitngaza kuwa, askari usalama wa nchi hiyo wamefanikiwa kumtia mbaroni gaidi huyo wa Daesh huko Talafar kufuatia uratibu waliofanya na kitengo cha kusimamia oparesheni huko magharibi mwa mkoa wa Nainawa, kaskazini mwa Iraq. Chinjachinja huyo wa kundi la kigaidi la Daesh ametiwa mbaroni ikiwa katika kuendelea oparesheni ya kuwasaka magaidi wa kundi hilo na mamluki wao. Gaidi huyo ambaye ni mwenyeji wa wilaya ya al Ayyadiyah huko Nainawa alikuwa akiendesha shughuli za kigaidi katika fremu ya tawi la Daesh kwa jina la al Jazeera.
Iraq mwaka 2017 ilitangaza kulishinda kundi la Daesh baada ya kupigana nalo vita kwa muda wa miaka mitatu, hata hivyo mamluki na masalia ya kundi hilo la kitakfiri bado wametapakaa huku wakiendeshesha jinai na hujuma mbalimbali dhidi ya wananchi wa Iraq katika baadhi ya maeneo ya mikoa ya Diyala, Kirkuk, Nainawa, Salahuddin, al Anbar na mji mkuu Baghdad.
Askari usalama wa Iraq wanafanya kila linalowezekana ili kuwaangamiza kabisa masalia ya magaidi hao wa Daesh katika maeneo hayo tajwa huko Iraq.