Wananchi wa Bahrain waandamana na kusisitiza kuachiliwa huru Sheikh Ali Salman
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i7024-wananchi_wa_bahrain_waandamana_na_kusisitiza_kuachiliwa_huru_sheikh_ali_salman
Wananchi wa Bahrain jana Ijumaa walifanya maandamano makubwa dhidi ya utawala wa kifalme wa nchi hiyo na kusisitiza kuendeleza mapinduzi yao.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 13, 2016 23:22 UTC
  • Wananchi wa Bahrain waandamana na kusisitiza kuachiliwa huru Sheikh Ali Salman

Wananchi wa Bahrain jana Ijumaa walifanya maandamano makubwa dhidi ya utawala wa kifalme wa nchi hiyo na kusisitiza kuendeleza mapinduzi yao.

Maandamano hayo yaliyofanyika baada ya Sala ya Ijumaa yalishuhudia waandamanaji hao wakipiga nara za kutaka kuachiliwa huru Sheikh Ali Salman Kiongozi wa Harakati ya al-Wifaq na wananchi wafungwa wengine wote waliotiwa gerezani kwa sababu ya imani zao za kidini.

Taarifa zaidi zinasema kuwa, maandamano hayo yalifanyika kaskazini magharibi mwa Bahrain na kuwashirikisha maelfu ya watu.

Waandamanaji hao wakiwa wamebeba mabango na maberamu wametoa wito wa kuachiliwa huru wananchi wote wa Bahrain wanaoshikiliwa katika magereza ya nchi hiyo kwa sababu ya imani zao za kidini akiwemo Sheikh Ali Salman kiongozi wa Harakati ya Wananchi ya al-Wifaq.

Sheikh Ali Salman alitiwa mbaroni Disemba mwaka 2014 kwa tuhuma za kufanya njama za kuuangusha utawala wa kifalme wa nchi hiyo na kushirikiana na madola ya kigeni. Sheikh Ali Salman na harakati yake ya al-Wifaq walikana tuhuma hizo.

Bahrain imekuwa uwanja wa malalamiko ya wananchi dhidi ya siasa za utawala wa kidikteta wa Aal Khalifa tangu mwaka 2011 hadi sasa.

Makumi ya watu wameuawa hadi sasa na maelfu ya wengine kujeruhiwa kufuatia ukandamizaji wa vikosi vya usalama vya utawala wa al-Khalifa dhidi ya raia wa nchi hiyo wanaotaka mabadiliko ya kisiasa na uhuru wa kutoa maoni.