Idadi ya askari wa Israel wanaojiua imeongezeka ghafla
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i85036-idadi_ya_askari_wa_israel_wanaojiua_imeongezeka_ghafla
Duru za Kiebrania zimeripoti ongezeko la idadi ya askari wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel waliojiua katika kipindi cha miezi sita ya kwanza ya mwaka huu wa 2022.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jun 22, 2022 07:56 UTC
  • Idadi ya askari wa Israel wanaojiua imeongezeka ghafla

Duru za Kiebrania zimeripoti ongezeko la idadi ya askari wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel waliojiua katika kipindi cha miezi sita ya kwanza ya mwaka huu wa 2022.

Wataalamu wa Kizayuni wametangaza kuwa, kuongezeka idadi ya askari wa jeshi la Israel wanaojiua kunadhihirisha ongezeko la matatizo ya kinafsi na kiakili waliyonayo askari hao na kwamba idadi ya wanajeshi walioomba kupatiwa huduma za ushauri wa kisaikolojia imeongezeka mno.

Televisheni ya Russia al Yaum imeinukuu chaneli moja ya kizayuni ikitangaza kuwa, katika miezi sita ya kwanza ya mwaka huu, askari 11 wa jeshi la Israel wamechukua hatua ya kujiua, wakati idadi sawa na hiyo ilishuhudiwa katika kipindi chote cha mwaka uliopita wa 2011.

Askari wa kizayuni wanawalilia wenzao waliojiua

Yanif Ashur, mkuu wa idara ya rasilimaliwatu katika jeshi la utawala wa Kizayuni amesema, "tunataka tufanye mazungumzo na wakuu wa kitengo cha afya ya saikolojia ili kuchunguza na kubaini sababu za ongezeko hili linalotiwa wasiwasi".

Kabla ya hapo duru za kizayuni ziliwahi kukiri kwamba askari wa jeshi la Israel wamekumbwa na tatizo la mkanganyo na mfadhaiko na zikaripoti kuwa maafisa kadhaa wametoroka jeshini kutokana na kuwahofu wanamapambano wa Muqawama.../