UAE: Tumo mbioni kupeleka balozi wetu Tehran
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i85952-uae_tumo_mbioni_kupeleka_balozi_wetu_tehran
Mshauri wa masuala ya kidiplomasia wa Rais wa Muungano wa Falme za Kiarabu (UAE) Anwar Qarqash amesema nchi yake iko mbioni kumrejesha balozi wake mjini Tehran.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 16, 2022 21:45 UTC
  • UAE: Tumo mbioni kupeleka balozi wetu Tehran

Mshauri wa masuala ya kidiplomasia wa Rais wa Muungano wa Falme za Kiarabu (UAE) Anwar Qarqash amesema nchi yake iko mbioni kumrejesha balozi wake mjini Tehran.

Katika miaka kadhaa nyuma, uhusiano wa Iran na Imarati (UAE) ulikuwa umejengeka katika mabadilishano ya kiuchumi na kibiashara, lakini Abu Dhabi, ambayo ni mji mkuu wa kisiasa wa muungano huo wa falme za Kiarabu imekuwa mara nyingi ikifuata mkondo inaopita Saudi Arabia.

Baada ya kuvunjika uhusiano wa Saudi Arabia na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Imarati iliamua kufuata sera za kihasama za Riyadh dhidi ya Tehran, ikaamua kushusha uhusiano wake wa kidiplomasia na Iran kutoka ngazi ya ubalozi hadi ubalozi mdogo.

Akizungumza katika mahojiano na televisheni ya CNN, Qarqash amesema: Imarati iko tayari kutoa mashirikiano kwa mpango uliopendekezwa na Marekani, lakini haiilengi nchi yoyote katika eneo.

Mshauri huyo wa masuala ya kidiploamsia wa Rais wa Muungano wa Falme za Kiarabu akaongezea kwa kusema: "Ninaiashiria hasa Iran, ni kwamba tumo mbioni kupeleka balozi wetu Tehran".

Aidha, amesisitiza kuhusu ulazima wa kuondolewa mivutano na kuendelezwa ushirikiano wa kiuchumi na Iran.

Kabla ya kauli hiyo ya Qarqash, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amir-Abdolahian, naye pia alieleza wakati wa ziara fupi aliyofanya hivi karibuni mjini Abu Dhabi kwamba, ukurasa mpya umefunguliwa katika uhusiano wa Iran na Muungano wa Falme za Kiarabu.../