Wanajeshi wa Kizayuni wavamia Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i86042-wanajeshi_wa_kizayuni_wavamia_ukingo_wa_magharibi_wa_mto_jordan
Wanajeshi wai utawala ghasibu wa Israel wameyavamia maeneo mbalimbali ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan katika kuendeleza uhasama wao dhidi ya raia wa Palestina.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 19, 2022 03:42 UTC
  • Wanajeshi wa Kizayuni wavamia Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan

Wanajeshi wai utawala ghasibu wa Israel wameyavamia maeneo mbalimbali ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan katika kuendeleza uhasama wao dhidi ya raia wa Palestina.

Wanajeshi wa utawala wa Kizayuni leo wamevamia maeneo tofauti ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na kuwatia nguvuni Wapalestina wanne katika eneo la al Yamun magharibi mwa mji wa Jenin. 

Tovuti ya Shihab News imeripoti kuwa, Wapalestina 12 wametiwa nguvuni kufuatia uvamizi mkubwa wa wanajeshi wa Kizayuni huko Ukingo wa Magharibi ambao umeanza tokea leo Jumanne. 

Duru za Kizayuni aidha zimeripoti kuwa, jeshi la utawala wa Kizayuni limeshadidisha uvamizi na ukandamizaji dhidi ya raia wa Palestina wa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan baada ya safari ya Rais Joe Biden wa Marekani katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu. 

Katika upande mwingine, wanajeshi wa Israel leo wamekivamia kwa mara ya 204 kijiji cha al Araqib kusini mwa Palestina inayokaliwa kwa mabavu na kusababisha madhara kwa kijiji hicho.