11 Wauawa katika mlipuko wa bomu Istanbul
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i8707-11_wauawa_katika_mlipuko_wa_bomu_istanbul
Mji wa Istanbul nchini Uturuki umekumbwa na mlipuko wa bomu ambapo watu 11 wameripotiwa kupoteza maisha na wengine 36 kujeruhiwa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 07, 2016 09:50 UTC
  • 11 Wauawa katika mlipuko wa bomu Istanbul

Mji wa Istanbul nchini Uturuki umekumbwa na mlipuko wa bomu ambapo watu 11 wameripotiwa kupoteza maisha na wengine 36 kujeruhiwa.

Imearifiwa kuwa gari lililokuwa limesheheni bomu limelipuka katika eneo la Vezneciler karibu na kituo cha mabasi. Bomu hilo linaaminika kuripuliwa kwa njia ya remote control kwani mlipuko umejiri wakati basi la polisi lilipopita hapo.

Mili ya risasi ilisikika punde baada ya mlipuko huo uliojiri masaa ya asubuhi yanayokuwa na msongamano mkubwa. Hakuna kundi lololote lililodai kuhusika na mlipuko huo lakini wanagambo wa Kikurdi, magaidi wa ISIS au Daesh na watu wenye itikadi kali za mrengo wa kushoto wamekuwa wakitekeleza mashambulizi nchiini Uturuki katika miezi ya hivi karibuni.

Milipuko hiyo ya mabomu imepelekea idadi ya watalii kupungua sana Uturuki na hivyo kutoa pigo kwa uchumi wa nchi hiyo.