Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa aikosoa Saudia
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i8854-katibu_mkuu_wa_umoja_wa_mataifa_aikosoa_saudia
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa mashinikizo yanayotolewa na Saudia kuhusu hatua yake ya kukiuka haki za watoto huko Yemen ni jambo lisiloweza kuhalalishwa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 09, 2016 23:16 UTC
  • Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa aikosoa Saudia

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa mashinikizo yanayotolewa na Saudia kuhusu hatua yake ya kukiuka haki za watoto huko Yemen ni jambo lisiloweza kuhalalishwa.

Ban Ki-moon Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amekosoa mashinikizo yasiyohalalishika yanayotolewa na Saudia kutoka na msimamo wa umoja huo dhidi ya ukiuakaji wa haki za watoto wa Yemen zinazofanywa na Saudia. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema Saudi Arabia imetishia kuukatia Umoja wa Mataifa misaada ya kifedha iwapo jina lake halitaondolewa kwenye orodha nyeusi ya umoja huo kutokana na hatua yake ya kukiuka haki za watoto huko Yemen. Wakati huo huo makundi 20 ya kutetea haki za binadamu likiwemo Shirika la Human Rights Watch limemtaka Ban Ki-moon kuliweka tena jina la Saudi Arabia katika faharasa nyeusi ya Umoja wa Mataifa kwa hatua yake ya kukanyaga vibaya haki za watoto huko Yemen.