Wananchi wa Ireland waonyesha mshikamano na uungaji mkono kwa Wapalestina
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i88574-wananchi_wa_ireland_waonyesha_mshikamano_na_uungaji_mkono_kwa_wapalestina
Wananchi wa Ireland wamebeba na kupeperusha bendera ya Palestina mbele ya wanasoka wa timu ya utawala wa Kizayuni wa Israel kuonyesha mshikamano na uungaji mkono wao kwa wananchi wa Palestina.
(last modified 2026-07-02T04:13:23+00:00 )
Sep 26, 2022 00:06 UTC
  • Wananchi wa Ireland waonyesha mshikamano na uungaji mkono kwa Wapalestina

Wananchi wa Ireland wamebeba na kupeperusha bendera ya Palestina mbele ya wanasoka wa timu ya utawala wa Kizayuni wa Israel kuonyesha mshikamano na uungaji mkono wao kwa wananchi wa Palestina.

Ireland ni moja ya nchi za Ulaya ambazo zimekuwa zikishuhudia mara kwa mara  harakati za kuonyesha mshikamano na uungaji mkono kwa kadhia ya Palestina.
Hivi karibuni Waziri Mkuu wa Ireland Micheal Martin alikosoa harakati haramu za utawala wa Kizayuni zinazohusiana na upanuzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni na kusema kuwa, ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi unavuruga uhusiano wa kijiografia wa vitongoji hivyo na Palestina.
Micheal Martin

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Mehr mashabiki wa soka nchini Ireland wamekusanyika mbele ya kambi ya timu ya soka ya utawala haramu wa Kizayuni ya vijana chini ya umri wa miaka 21 na kupeperusha bendera ya Palestina.

Timu ya soka ya utawala haramu wa Israel ilikuwa imeelekea Ireland kushiriki mechi za hatua ya awali ya michuano ya kutafuta bingwa wa Mataifa ya Ulaya.../