Msemaji wa Jihad Islami: Utawala ghasibu haupasi kutahini subira ya muqawama
Msemaji wa harakati ya Jihad Islami ya Palestina ametangaza kuwa machaguo yote yanayoweza kutumika ikiwemo jibu la kijeshi yapo mezani.
Tariq Izzudin ambaye ni msemaji wa harakati ya Jihad Islami ya Palestina ameema kuwa, utawala wa Kizayuni utambue kuwa muqawama kamwe hautakaa kimya na utawala huo haupasi kutahini subira ya makundi ya muqawama ikiwemo harakati ya Jihad Islami.
Izzudini ameeleza kuwa, uvamizi na mashambulizi yanayofanywa na walowezi wa Kizayuni wanaosadiwa na wanajeshi wa Kizayuni katika msikiti wa al Aqsa ni katika muendelezo wa sera za uvamizi za wanajeshi wa Kizayuni dhidi ya matukufu ya Kiislamu; ambayo yanahitaji uungaji mkono wa kweli na wa dhati.
Msemaji wa Jihad Islami amesisitiza kuwa tunavihesabu vitendo hivyo vya kigaidi kuwa ni kushadidisha mashambulizi na hatua hatari ambavyo wanajeshi Wazayuni wanahusika kikamilifu na maafa na taathira zake. Amesema uvamizi na hujuma hizo za wanajeshi wa Israel na walowezi za Kizayuni kamwe hazitazima irada na azma ya waumini wanaokaa itiqaf katika msikiti wa al Aqsa.
Wanajeshi wa utawala haramu jana waliivamia kambi ya wakimbizi wa Kipalestina katika mji wa Jenin katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan; ambapo mapigano makali yalizuka kati ya wanajeshi wa Israel na Wapalestina. Vijana kadhaa wa Kipalestina waliuawa shahidi na wengine wasiopungua 44 walijeruhiwa katika mapigano hayo ya jana huko Jenin.