Israel yaendelea kuwatia nguvuni Wapalestina kaskazini mashariki mwa Quds
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i89062-israel_yaendelea_kuwatia_nguvuni_wapalestina_kaskazini_mashariki_mwa_quds
Wanajeshi wa Kizayuni wameendelea na hatua zao za kiuhasama ambapo wamewatia nguvuni raia kadhaa wa Palestina huko Quds inayokaliwa kwa mabavu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 09, 2022 04:18 UTC
  • Israel yaendelea kuwatia nguvuni Wapalestina kaskazini mashariki mwa Quds

Wanajeshi wa Kizayuni wameendelea na hatua zao za kiuhasama ambapo wamewatia nguvuni raia kadhaa wa Palestina huko Quds inayokaliwa kwa mabavu.

Duru za ndani ya Palestina zinaarifu kuwa, wanajeshi ghasibu wa Israel jana usiku waliwatia nguvu vijana wa Kipalestina wasiopungua wanne karibu na kituo cha upekuzi cha Anata kaskazini mashariki mwa mji wa Quds unaokaliwa kwa mabavu.  

Wakati huo huo mabarobaro wawili wa Kipalestina kwa majina ya Mahmoud as-Sous na Ahmad Mohammad Hossein Daraghmeh wameuliwa shahidi na wanajeshi ghasibu wa Kizayuni wakati wanajeshi hao walipovamia kambi ya wakimbizi ya Jenin katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.  

Hali ya mambo katika siku za karibuni katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina khususan huko Ukingo wa Magharibi si ya kawaida kabisa ambapo wanamuqawama wa Kipalestina wakitumia kila nyenzo wamejibu jinai zisizohesabika za Israel; suala ambalo limewaweka Wazayuni maghasibu katika hali ngumu.