Hamas:Tutazidisha oparesheni za muqawama dhidi ya Wazayuni
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i97082-hamas_tutazidisha_oparesheni_za_muqawama_dhidi_ya_wazayuni
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imesema kuwa taifa shujaa la Palestina kamwe halitaacha kutoa jibu kwa jinai za maghasibu wa Kizayuni na kuwa litazidisha oparesheni zake dhidi ya jinai hizo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 07, 2023 03:26 UTC
  • Hamas:Tutazidisha oparesheni za muqawama dhidi ya Wazayuni

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imesema kuwa taifa shujaa la Palestina kamwe halitaacha kutoa jibu kwa jinai za maghasibu wa Kizayuni na kuwa litazidisha oparesheni zake dhidi ya jinai hizo.

Diyar Omar kijana wa Kipalestian aliyekuwa na umri wa miaka 20 jana aliuliwa shahidi na mlowezi mmoja wa Kizayuni katika kijiji cha Sandala katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu. 

Shirika la habari la Palestina limeripoti kuwa, Hamas jana usiku ilitoa taarifa ikisisitiza kuwa itashadidisha oparesheni za kimuqawama ili kulipiza kisasi damu ya mashahidi shujaa wa Palestina khususan kijana huyo wa miaka 20 aliyeuliwa na mlowezi wa Kizayuni kwa kupigwa risasi.  

Hamas imetangaza kuwa damu ya raia wa Palestina sio nafuu, na adui atalipa gharama kubwa kwa hatua hiyo. Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imewatolea wito wananchi shupavu wa Palestina katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu kukabiliana na wanajeshi wa Kizayuni na vitendo vya unyanyasaji vya walowezi wa Kizayuni na kulipiza kisasi damu ya kijana huyo wa Kipalestina na mashahidi wengine.  

Hamas pia imewataka Wapalestina kujikusanya na kuelekea katika Msikiti wa al Aqsa ambao ndio mlengwa mkuu wa wimbi kubwa la kulifanya eneo hilo kuwa la Kiyahudi na kulivunjia heshima. 

Jana asubuhi wanajeshi wa utawala haramu wa Israel walivamia kambi ya wakimbizi wa Kipalestina ya Nur Shams mashariki mwa mji wa Tul-Karam katika ukingo wa Magharibi wa mto Jordan na kuwaua shahidi vijana wawili wa Kipalestina walio kuwa na miaka 22. 

Mashahidi hao walipoteza maisha kutokana na majeraha ya risasi walizopigwa vifuani mwao, shingoni na tumboni. Haya ni kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Palestina. 

Vijana wawili wa Kipalestina waliouliwa shahidi katika kambi ya Nour Shams