Mwanadiplomasia wa zamani wa Uswidi: Apartheid itasababisha kuanguka kwa Israel
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i98060-mwanadiplomasia_wa_zamani_wa_uswidi_apartheid_itasababisha_kuanguka_kwa_israel
Mwanasiasa na mwanadiplomasia wa zamani wa Uswidi amejibu matamshi ya viongozi wa utawala wa Kizayuni katika mkutano wa Herzliya akisisitiza kuwa, ubaguzi wa apartheid unaisukuma Israel kuelekea shimoni.
(last modified 2026-07-11T07:59:36+00:00 )
May 27, 2023 02:36 UTC
  • Carl Bildt
    Carl Bildt

Mwanasiasa na mwanadiplomasia wa zamani wa Uswidi amejibu matamshi ya viongozi wa utawala wa Kizayuni katika mkutano wa Herzliya akisisitiza kuwa, ubaguzi wa apartheid unaisukuma Israel kuelekea shimoni.

Mkutano uliofanyika hivi majuzi huko Herzliya, ulijadilii suala la usalama na vitisho vinavyouzunguka utawala wa Kizayuni, ambako Herzi Halevi, Mkuu wa majeshi ya Israel, alikariri madai yake dhidi ya Iran, na kuzungumzia ugumu wa vita na harakati ya Hizbullah ya Lebanon.

Kwa mujibu wa tovuti ya habari ya Sama, Carl Bildt alisema: "Ukweli kwamba suala la Wapalestina halikujadiliwa katika mkutano wa Herzliya unaonyesha kuwa Israel haina sera ya wazi kuhusiana na masuala muhimu zaidi yanayogusa mustakbali wake na kwamba utawala huo kamwe hautaendelea kuwepo katika kivuli cha sera za ubaguzi wa rangi, apartheid."

Carl Bildt alikuwa waziri mkuu wa Uswidi katika miaka ya tisini na waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo kuanzia 2006 hadi 2014.

Mwanasiasa huyo wa Uswidi pia ameandika wakati akiondoka Tel Aviv kwamba: "Asia Magharibi sasa inakuwa maabara kwa ulimwengu wa baada ya Marekani."

Siasa za ubaguzi wa kimbari na ukandamizaji wa utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina zimethibitishwa na duru za kimataifa. Hivi karibuni Jean-Paul Lecoq, mbunge wa Bunge la Taifa la Ufaransa alikosoa mienendo ya utawala wa Kizayuni ya ukandamizaji wake katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na kusisitiza kuwa: Kisheria, Wapalestina wako chini ya utawala wa kibaguzi (wa apartheid).