Doha: Tunaunga mkono mgogoro wa Syria kupatiwa ufumbuzi wa kudumu
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i98570-doha_tunaunga_mkono_mgogoro_wa_syria_kupatiwa_ufumbuzi_wa_kudumu
Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar amesema kuwa Doha inataka mgogoro wa Syria utatuliwekwa uadilifu na kwamba inaunga mkono utatuzi wa kisiasa katika uwanja huo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 09, 2023 03:12 UTC
  • Doha: Tunaunga mkono mgogoro wa Syria kupatiwa ufumbuzi wa kudumu

Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar amesema kuwa Doha inataka mgogoro wa Syria utatuliwekwa uadilifu na kwamba inaunga mkono utatuzi wa kisiasa katika uwanja huo.

Sheikh Muhammad bin Abdulrahman Al Thani ameeleza kuwa nchi hiyo haina tatizo lolote na Syria na kwamba inataka mgogoro wa nchi hiyo upatiwe ufumbuzi kwa njia za kisiasa. Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar amesisitiza kuwa Doha inataka mgogoro wa Syria utatuliwe kwa uadilifu na kwamba wanaunga mkono njia za kisiasa ambazo zitawaridhisha watu wa nchi hiyo. 

Majid bin Muhammad al Ansari Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar mwezi uliopita alikaribisha na kutangaza kuwa Qatar inaunga mkono jitihada za nchi za Kiarabu za kutatua mgogoro wa Syria na kusisitiza kuwa njia hizo za utatuzi zinapasa kufungamana na hatua chanya na kutatuliwa matakwa ya wananchi wa Syria.   

Syria ilrejeshewa  kiti chake katika Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League) mwezi Mei mwaka huu kufuatia makubaliano ya Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi wanachama katika mkutano wa dharura wa  ulioitishwa kujadili suala hilo.

Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League)