Majasusi wa Israel wawafanyia ujasusi mkubwa wananchi wa nchi za Kiarabu
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i98652-majasusi_wa_israel_wawafanyia_ujasusi_mkubwa_wananchi_wa_nchi_za_kiarabu
Tovuti ya habari ya ICAD imefichua kuwa, utawala wa Kizayuni unawafanyia ujasusi mkubwa watumiaji Waarabu wa mitandao wa kijamii ikiwa ni pamoja na kudukua mambo wanayoyatuma kwenye mitandao hiyo ili kupata watu wa kuwatumia kwa maslahi yao.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 11, 2023 07:57 UTC
  • Majasusi wa Israel wawafanyia ujasusi mkubwa wananchi wa nchi za Kiarabu

Tovuti ya habari ya ICAD imefichua kuwa, utawala wa Kizayuni unawafanyia ujasusi mkubwa watumiaji Waarabu wa mitandao wa kijamii ikiwa ni pamoja na kudukua mambo wanayoyatuma kwenye mitandao hiyo ili kupata watu wa kuwatumia kwa maslahi yao.

Mashirika ya kijasusi ya utawala wa Kizayuni yametenga fedha nyingi za kuwarubuni na kuandaa rasilimali watu kwa ajili ya kuwatumia kwenye masuala ya kijasusi. 

Tovuti hiyo imeandika katika ukurasa wa Twitter kwamba, kundi la «Lead Capital Holding (TCH) Limited» linafanya kazi rasmi na kwa mujibu wa sheria katika Muungano wa Nchi za Kiarabu (Imarati) na kwamba mashirika tangu na kundi hilo yanatoa mafunzo wa bure kwa vijana wa UAE na wengineo.

Ripoti hiyo imeongeza kuwa, kundi hilo linaongozwa na Mzayuni ajulikanaye kwa jina la Roei Gavish na mashirika yanayounda kundi hilo yanadukua taarifa za watumiaji wa aplication mbalimbali za kijamii za wanaozungumza lugha ya Kiarabu.

Imefichuliwa kuwa utawala wa Kizayuni unafanya ujasusi mkubwa dhidi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii wa lugha ya Kiarabu.

 

Ripoti hiyo imeongeza kuwa, Mzayuni huyo ameanzisha shirika la «Tplus Technologies» ambalo linatoa huduma za fedha katika mitandao ya kijamii.

Taarifa ya tovuti hiyo imeongeza kuwa, uchunguzi unaonesha kuwa, shirika la «Tplus Technologies» linafanya njama za kupenya kwenye mifumo ya usalama, ya kijeshi na ya kiserikali. 

Ripoti hiyo imeongeza kuwa, taasisi mbili za «Evest» na «Mister Market Pro» zinafanya kazi kama mtandao mkubwa wa "brand" za biashara ambazo zinaendeshwa na wafanyabiashara Wazayuni. Kanali hizo zinafanya udukuzi wa kurasa za mitandao ya kijamii za watumiaji wa lugha ya Kiarabu wanaoishi Qatar na nchi nyingine za Kiarabu za Ghuba ya Uajemi na kuiba taarifa zao muhimu.