HAMAS yalaani upanuzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni Quds
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i98768-hamas_yalaani_upanuzi_wa_vitongoji_vya_walowezi_wa_kizayuni_quds
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imelaani vikali uamuzi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wa kupanua ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni wa Israel mashariki mwa Quds tukufu inayokaliwa kwa mabavu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 14, 2023 07:36 UTC
  • HAMAS yalaani upanuzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni Quds

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imelaani vikali uamuzi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wa kupanua ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni wa Israel mashariki mwa Quds tukufu inayokaliwa kwa mabavu.

Taarifa ya HAMAS mbali na kulaani uamuzi huo wa Israel imeutaka Umoja wa Mataifa kutekeleza majukumu yake kimataifa kuhusiana na kusitisha ujenzi wa vitongozi vya walowezi wa Kizayuni unaofanya na utawala ghasibu wa Israel huko Palestina.

Muhammad Hammadah, msemaji wa Harakati ya Mapambani ya Kiislamu ya Palestina HAMAS ameutaja uamuzi huo wa Israel kuwa ni jinai na uangamizaji kizazi unaofanywa na serikali ya sasa ya Benjamin Netanyahu dhidi ya taifa la Palestina.

Afisa huyo wa Hamas amekosoa vikali pia misimamo ya jamii ya kimataifa na kusisitiza kuwa, udhaifu na utepetevu huu ndio unaoupa kiburi utawal wa Kizayuni wa Israel cha kuendelea kutenda jinai zaidi sambamba na kukiuka bila woga maazimio na sheria za kimataifa.

Vitongoji haramu vya walowezi wa Kizayuni

 

Radiamali hiyo ya Hamas inakuja baada ya utawala wa Kizayuni wa Israel kutangaza juzi kwamba, una mpango wa kujenga nyumba mpya 1,700 katika kijiji cha Beit Hanina kilichoko kaskazini mwa Quds inayokaliwa kwa mabavu.

Katika miezi ya hivi karibuni vitendo vya hujuma na uvamizi wa walowezi wa Kizayuni katika maeneo ya Wapalestina hususan katika Msikiti wa al-Aqswa vimeongezeka mno.

Madola ya Magharibi yamekuwa yakikosolewa kutokana na himaya na uungaji mkono wake kwa utawala ghasibu wa Israel na hata wengi wanaamini kuwa, himaya hiyo ndiyo inayoupa kiburi utawala huo ghasibu.